Na Sir Carlos Mwigani:
¶KISA kimoja kizito na Cha kusisimua kilichotokea nchini Thailand Tangu miaka ya 2021 Toa 1961 iliyopita katika Enzi za utawala wa Ki Mono" kwa Mzee wa makamu sana Aitwae "Tanzacarlomwizanziloga" mwenye miaka isiyozidi na Isiyopungua 50 na Penta,kwenye "Cold Civil war" yaani (vita baridi vya wenyewe kwa wenyewe) vya Kisiasa, Kiuchumi na kijamii.Ndicho kilinifanya ni itazame upya na kimapana zaidi Siasa ya "TANZANIA MPYA".
Ipo hivi Kwa ufupi ...!
✍🇹🇿 Tanzania Tangu Kuumbwa kwake kisiasa 1961 na waasisi wetu akina hayati Baba wa Taifa J.K Nyerere, Sheikh Aman Abeid Karume, Rashidi Kawawa, Oscar Salathiel Kambona,Moringe Sokoine, Bibi Titi, Eliya Chipaka, Prisca Chiombola, Grey Mattaka,Comrade Hanga,na wengine weengi; Mpaka miaka ya 1995 tulipoingia katika mfumo wa Vyama vingi vya Siasa (NCCR_Mageuzi ya Agustine MREMA, CUF ya akina James Mapalala, CHADEMA ya akina Edwin Mtei na Bob Makani pia vyama vingine kamavile,TLP, TADEA,UPDP,CHAUSTA,UDP, CHAUMA,na baadae tukawa na ACT_WAZALENDO ).
Ambapo tukapitishwa na tawala za Viongozi Mbalimbali Akiwemo Mzee wetu Ally Hassan mwinyi ('mzee wa Ruksa'), Mhe;William Benjamini Mkapa, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Mpaka sasa tunae>{ Mtu Makini ,Jemedali la vita,Mchapakazi na Mwanasiasa za kizalendo Si mwingine ni> Dkt John Pombe Joseph Magufuli .
Sasa Ni lazima tufanye Tathimi za kitafiti na kitaalamu Ili kujua Kisiasa wapi tumetoka, wapi tulipo na Tunakwenda wapi katika kufanya mapinduzi makubwa ya "siasa za kizalendo" na sio zile siasa za Kiulimbwende kama taifa; kwa kubaini pia kwanini tuliishi hivyo wakati huo. Kwasababu Siasa zetu ndio msingi mkubwa wa Kukua Kiuchumi, kijamii, na kitamaduni ambapo mjumuisho wa yote hayo Tangu Enzi za Nyerere tunapaswa kujifunza na kubadilika kwa Mustakabali wa maisha ya Wasakatonge wengi Tunaowaongoza.
✍🇹🇿{Howard Zinn >
Mwanafalsafa wa kijamii kutoka Ardhi ya Amerika ya kaskazini mwanzoni mwa mwaka 2000, aliandika katika kitabu chake cha {"Declaration of Independence"} nanukuu anasema> " Politics is pointless if it does nothing to enhance the beauty of our lives" mwisho wa kunukuu. ' Yaani siasa itakuwa si kitu ikiwa haitapendezesha maisha yetu.
Ikiwa katika nyakati tofauti siasa za Tanzania kwa Viongozi mbalimbali waliopita zimekuwa ni chachu ya maendeleo tuyaonayo hilo nakili lipo wazi lakini Lazima pia tukubali ukweli usiopingika kuwa, Umri wa Tanzania umekuwa ni mkubwa kuliko ukilinganisha na maendeleo yaliyopo, Hii nadhani ni kwasababu Wapo Wanasiasa baadhi wa vyama vyote Nchini Tangu 1960's waliishi ile dhana isemayo siasa ni mchezo tu mchafu ("Dirty game") na kuiacha kwa 60% siasa ya Kizalendo Amini nakwambia hili mpaka sasa Linazidi kututafuna kama Taifa Huru.
Hatahivyo :
Tanzania kabla hatuja angazia jambo hili kihistoria katika kurejea Matukio ya kiushahidi Nchini, na zile Nukuu za "Great thinkers" Vitakavyoonyesha na kuthibitisha udhaifu wetu kisiasa Nchini kiasi ambacho hata mataifa ya wenzetu na mabeberu yanatung'ong'a bure Ebu tuielewe zaidi hii dhana ya "Mapinduzi ya siasa za kizalendo"niitakayo Tz, ili kubaini na kupima ukweli wa kichambuzi uliopo:
✍🇹🇿 Ni yale Mageuzi ya dhati Kiitikadi, Kifikra, Kimtazamo/kimawazo, Kiutendaji na Kimaono thabiti Kuambatana na Upendo uliotukuka wa Nchi yako bila kushawishiwa, kupangiwa au kuamriwa Kimkakati na Mtu,CHAMA CHA SIASA,Taasisi,Shirika,au Taifa Fulani Nje na Ndani ya Nchi .👆👆Huu ni mtazamo wangu tu juu ya dhana ya " Mapinduzi ya siasa za kizalendo" Kitu ambacho ninashauri Wanasiasa wote wa Tanzania Kurejerea haya kupitia Makala hii Kwa UMMA : Sasa Kwa Utajiri wa maarifa zaidi ya haya ninayoyang'amua kwenu wasomaji wa makala zangu Tamu tusome zaidi Vitabu kama vile "Why Africa is Poor? "By Greg Mills,) " "Tujisahihishe"By Mwl J.k nyerere, )" Beyond Government"By Eddie Richie,) pia hata "mapinduzi Vijijini"By chigaithan).
✍TZ Katika Maktaba ya Ubongo wangu naikumbuka Tanzania ya J.K Nyerere ambapo miaka ya 1967 nchi yetu ilipo Tangaza lile "Azimio la Arusha" Kupitia Siasa ya Ujamaa na kujitegemea Mfumo uliotumika hata na Nchi kama vile Urusi, na China kwa Mao, ambao uliopendezwa sana na Mwl wakati huo.Japo mwenendo wa kisiasa Nchini wakati huo haukuwa mzuri kwani bado nchi yetu pamoja na idadi ya watu kuwa ndogo ilikuwa inakabiliwa na Matatizo matatu yaliyobainishwa na Mwl yaani "Ujinga, Umaskini na Magonjwa" , Lakini pamoja na maono ya dhati ya Mwl katika kuujenga uchumi wa Nchi kwa wakati huo kupitia uwekezaji sekta ya Elimu, Kilimo, na Viwanda vidogovido (SIDO), na Vikubwa Wapo watu waliompinga sana kwenye utawala wake katika siasa ya Ujamaa na kujitegemea, nadhani Tutakumbuka hata miaka ya 1964 inasemekana waziri wake mkuu bwana Oscar Kambona, akina Bibi Titi, comrade Hanga na wengine wengi walioambatana nae walipotaka kufanya jaribio la kimpindua Baba yetu wa Taifa ambapo baada ya jaribio hilo kufeli Kambona aliamua kwenda Uhamishoni Kenya kisiasa na baadae Uingereza.
Kwahiyo hii inaonesha picha ya kwamba Tanzania siasa za Upinzani zilisha anza muda mrefu japo tangu 1961_1995 bado tulikuwa katika mfumo wa Chama kimoja.Sasa hoja ya msingi hapa nikwamba akina Oscar Kambona na wengine wengi waliotuhumiwa katika Vitendo vya Uhaini, Rushwa, utakatishaji, na ubadhilifu wa mali za Umma ambao wengine walipotea kabisa, Je kupitia siasa zao walikuwa na mapenzi ya dhati katika Taifa lao.?,
Pili walifanya siasa za kizalendo bila kutumiwa?,Tatu Walikuwa ni wapinzani kwa maslahi ya Taifa au ni usakatonge tu.?Nne hawakuwa wauchu wa madaraka.? Nami naona lolote inaweza kuwa. Japo Uhalisia nikwamba Kisiasa wakati huo tulikuwa wachanga sana mana hata wasomi na wataalamu Walikuwa wachache Ndio maana UTASHI wa Mwl kuhifadhi rasilimali za Nchi kama vile Madini, Wanyama, na Ardhi ULITUKUKA na hata Baadae 1999, pale St Thomas hospital kabla ya kukata roho akatuachia usia wake wa Mwisho nanukuu
"Najua Nitakufa sitapona ugonjwa huu, Nawaacha Watanzania wangu najua watalia sana nami nitawaombea kwa Mungu, Naondoka nikiwa nimewaachia Taifa lenye Umoja na Amani,Wosia wangu kwao Waipende Nchi yao kama wanavyowapenda Mama zao,Wajue hawana Nchi nyingine zaidi ya Tanzania"
✍🇹🇿Mtiririko wa Mambo mengine mengi sana ya Kisiasa yasiyohabarishwa katika makala yangu hii katika Zile Enzi za Nyerere yalipita na wengine Tukasahau kabisa hata kama yapo yaliyo acha Furaha kwetu na Mengine "Donda ndugu": Sasa Hiyo yaweza ikawa sio hoja saana kwetu sisi wanaharakati wa "Mapinduzi ya kisiasa za kizalendoTanzania"kama Ilivyo kwa Jemedali mmoja ivi kutoka CHATO,(JPM). Hoja ya msingi hapa Nikwamba Matukio yote hayo Je nyinyi Wanasiasa wa TZ, ambao wengine wengi mimi nawaita wanasiasa Mchwara Je Mnajifunza nini kupitia Historia ya Nchi yetu.?, na yapi mnayafanya kuwa Fursa kwenu bila ya maslahi binafsi au Chama.?, je mmesahau kuwa Tanzania ni taifa huru kisiasa, kiuchumi na hata kijamii..? Hivyo hatuwezi Ludi zile Zama za kabla ya 1950's zama za kuamriwa Amriwa, Kujidharau na kuigaiga ( UKOLONI ).
📌
Hakika " Patriotism is Racism for the modern Era" Mwanasiasa wa kike maarufu sana nchi za Ubeberu >(Michelle Trumplet )maneno yake yanathibitika Tanzania.
✍Tanzania Kisiasa hatukuishia katika Dondoo hizo tu, La hasha..! Kwani historia yetu ilizidi kunifunza mengi ndani ya Miaka ya 1995_2005, ambapo pale CCM ilipomsimamisha mgombea wake Mhe: William Benjamini Mkapa ambapo kabla ya kuelekea Uchaguzi huo nilivutiwa sana na Maneno ya Mwl mwenzangu Hayati Baba wa Taifa Mwl J.k Nyerere nanukuu "Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyaona ndani ya CCM watayatafuta kwengine" Lakini katika nyakati hizohizo nakumbuka NCCR_Mageuzi ndicho Kilikuwa chama kinara Miongoni mwa Vyama vya Upinzani vilivyoibuka Nchini kama vile TLP, CHADEMA,na vingine Vingi, Ambapo NCCR_Mageuzi wenyewe wakampitisha Agustine Mrema kuipeperusha bendera ya Chama hicho ila Vingine havikuwa na Nguvu sana.Kwa ufupi ikawa hivo, Lakini Cha Ajabu zaidi Watanzania Wengi wanaofuatilia siasa, walitegemea kuona mabadiliko makubwa sana ndani ya Serikali yao kutokana na Vuguvugu la Upinzani lilivyoingia nchini, Na Kwa kiasi chake tuliona jitihada kubwa za Mkapa katika sekta ya Elimu, Biashara,Miundombinu,Afya, Viwanda.Nadhani hapa tutakumbuka hata ule mpango wa SHULE ZA KATA ni Sera ya Mkapa, VYUO VIKUU Vilijengwa,Hospitali za Rufaa, na mambo kadha wa kadha.Lakini Kisiasa Tulianza kushuhudia Ile Mogogoro mingi iliyojitokeza ndani ya Vyama vya Upinzani katika hamahama yao kwenda vyama vingine Mfano Agustine mrema kwenda TLP, akina Marando CCM. Pia kipindi hiki zile siasa za Matakwa ya mabeberu,binafsi/ uchumia tumbo,Umimi/udikteta, na Ufitina zilishika Dola , Nchi ikakosa wanasiasa wa Upinzani wakuaminika na Wananchi ili kupewa Ridhaa ya kuongoza Nchi vipindi vingine Kiasi ambacho CCM, na baadhi ya watu wachache wasio na uzalendo ndani yake Ikaendelea kupata KIKI :
✍🇹🇿Awamu ya utawala wa mzee wangu Kikwete 2005_2015, Sina haja ya kuzungumza saana kwani ndicho kipindi ambacho Wengi walihamasika kufuatilia mwenendo wa Siasa Nchini, Lakini wanasiasa wa Upinzani chini ya chama kilichojichukulia Umaarufu katika kipindi hichoo yaani CHADEMA, kikichuana na CCM iliyojaa wanasiasa Wazalendo na Wale wachache WACHUMIA Tumbo/Wasaliti wa Taifa Hakukuwa na mabadiliko kiviiile kisiasa.Kiasi ambacho 2015 Chadema ilipoitangazia Dunia kuwa pamoja na kwamba CCM ilikuwa ime hange sana wamekosa weledi wa Kiufundi mpaka kumpitisha Mgombea Uraisi kada aliyezaliwa, na kulelewa na CCM mda mrefu yaan Edward Lowassa Hakika huku Ni>("Kutema Big G kwa Karanga za kuonjeshwa") Japo hatukujua katika hili nn kilijificha "Nyuma ya Pazia' Binafsi nikiwa bado mdogo kielimu na kiuchambuzi kipindi hiko nikaanza kuwatafakari zaidi Wapinzani wa Tanzania,Pia Nikaanza kuielewa zaidi CCM je Ni Chama cha Namna gani.?Hapa najalibu kuwaeleza Kiuhalisia, na sio Ki itikadi. Kwasababu Lazima ifike hatua Tuone Taifa kama Taifa Tunafeli wapi kisiasa; Kwa maana Vyama vyote vya siasa vipo kwa Mujibu wa katiba ya Jamhuri Sura ya kwanza Ibara 3(1), Lakini Mbona Vyama hivi Vinashindwa kubadilisha mwenendo wao..? Na kuiabudu Hii "Siasa ya Kizalendo" ninayoitolea Maoni.?, Kwanini upinge kilakitu.?, pia kwanini Utumiwe.?, lakini kwanini baadhi yao Ndani ya Mfumo wa serikali Uwe Msifiaji tu nasio mtendaji.?,Uwe msaliti, Muongo,na mnafki.? Daah Mpaka chozi linanitoka katika hili:Am kweli Nimeamini maneno ya Mfalsasfa mmoja nchini Uganda "Habambiki habyalimana kuwa >{"Politician are a bread of the human race who believe they know every things"}.
✍🇹🇿Kulipokucha na kupambazuka 2015&2020 Chini ya Msukuma kutoka chato Tanzania, Wale watu wa Gadha ndo Waka anza kukumbuka shuka Ndipo sasa nikaanza kuiona ile Tanzania niliyoiota nikiwa Tumboni mwa mama yangu katika Mengi ninayoiwazia TANZANIA likiwemo na hili la Kuwa"Mwanasiasa wa kizalendo Nchini" Kama ilivyo kwa watu wachache sana Tanzania kipindi ambacho kidogo naanza kuiona Afueni kisiasa. Mana amini Pia nachokwambia kuwa, yote haya yanayonitoka Ubongoni ni Utashi wa Fikra zangu mpaka najiuliza mbona mimi ni kijana mdogo sana Kufanya Uchambuzi wa ki "PHD".kama huu.?
✍🇹🇿 Chagua Magufuli na sio CCM 2015,Ndio kipimo cha kwanza nilichoanza nacho kukitumia na kutaka ni ichunguze zaidi nini maana yake katika utendaji wa Kiserikali.?Kumbe Baadhi ya Wanasiasa wa CCM, CHADEMA, ACT_WAZALENDO, NCCR_MAGEUZI na vyama vingine vya Upinzani Baadhi yao mpaka sasa Hawajayazoea mabadiliko haya ya Gafla na kihistoria Katika kutambua kuwa 1)hakuna CCM ya akina flani.?2)Utendaji wa mambo yanayo onekana kwa wananchi ndio siasa ya kweli 3)Umoja wa kizalendo ni bora zaidi kuliko Ubinafsi 4)Hakuna Uhuru wa watu pasipo wajibu 5)Usiasa mwingi ni kikwako kikubwa katika utendaji na Maendeleo 6)Uongozi ni Utumwa na sio ufalme 7)Ujasiri,uchungu,utendaji, na utatuzi ndio kipimo cha Uzalendo na mambo kadhaa yanayohusiana na hayo.Lakini yote hayo yamekuwa ni mageni kwetu , Pia hata kama uzalendo kwanza ila Upinzani ni kipaumbele. Ndio maana mpaka sasa linalo onekana kuwa ni tatizo kwa Vyama vingine vya siasa ni ule Uhuru wao wa kuongeaongea ili kulinda Ugali lakini kuhusu Maendeleo Wanadai Wanayaona kabisa.Lakini katika hili yapo mengi sana ya Kuchambua ila nisikuchoshe kwasababu.?
To be Continue ........>>
Itaendelea ..........>>
MWISHO :
Niwasihi sana Wanasiasa wote wa Tanzania na Wananchi wote kuwa, Kwanza muisome vizuri makala hii na kuielewa, Pia Tutambue ya kuwa Siasa si vita vya Uadui ,Chuki, unafiki, usaliti,fitna, Umimi,na Ubinafsi bali ni Vita huru ya Kizalendo, Tukumbuke kuwa hatuna nchi nyingine kama Tanzania Tuipende :
Nimimi kijana mdogo sana katika Chambuzi za masuala ya Kisiasa,na Kijamii Nchini Tanzania :
Sir Carlos Mwigani:
CONTACT'S :
Email(sircarlosmwigani@gmail.com)
(Normal no;0763469828)
Whatsap no ;(0756513178)
Facebook page :(Sir Carlos Mwigani, normal Carlos mwigani).
Youtube :(Sir Carlos Mwigani)
Instagram :(Sircarlos Mwigani)
Twitter :(@Sir Carlos Mwigan)
Year's ( Youth of 23 year's Old):
Post a Comment