Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, Scolastica Gibore akitoa ushauri wake walipokuwa wakichangia mada iliyotolewa kwao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu wakati wa kongamano hilo jijini Dodoma.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tanga, Moses Kisibo naye akichangia maoni yake wakati wa kongamano hilo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Karagwe, Edina Kabyazi akielezea jinsi upungufu wa rasilimali watu na fedha vinavyokwamisha utekelezaji wa mikakati ya maendeleo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Karagwe, Edina Kabyazi akielezea jinsi upungufu wa rasilimali watu na fedha vinavyokwamisha utekelezaji wa mikakati ya maendeleo.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
WATAALAMU wa Maendeleo ya Jamii nchini, wamesema inawawia vigumu kutekeleza mikakati ya maendeleo kwa wananchi kutokana na upungufu wa rasilimali watu na fedha za kuendeshea shughuli za kila siku za halmashauri.
Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na wataalamu hao wakati wa kuchangia maoni na ushauri wao baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu kuzungumza nao kuhusu uwajibikaji na utekelezaji wa mikakati ya kuwaletea maendeleo wananchi jijini Dodoma leo. Ndugu, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video wataalamu hao wakitoa ushauri na maoni yao na jinsi Katibu Mkuu, Dk. Jingu alivyowajibu....
WATAALAMU wa Maendeleo ya Jamii nchini, wamesema inawawia vigumu kutekeleza mikakati ya maendeleo kwa wananchi kutokana na upungufu wa rasilimali watu na fedha za kuendeshea shughuli za kila siku za halmashauri.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
Post a Comment