Watoto wa marehemu Nditiye wakiongoza jeneza la mwili wa babao kuingia kwenye viwanja vya bunge.
Sehemu ya wabunge wakisubiri kutoa heshima za mwisho kwa munge mwenzao marehemu Nditiye.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akongoza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Nditiye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe marehemu Nditiye kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Nditiye ambaye amefia Hospitali ya Benjamin Mkapa Februari 12 alipopelekwa kupata tiba baada ya kugongwa na gari eneo la Nanenane, Dodoma mwanzoni mwa wiki.
Katibu wa Bunge,Dkt Steven Kagaigai akitoa heshima za mwisho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Jenista Mhagama akiweka shada la maua.
Kiongozi wa wabunge walio wachache bungeni, Sophia Mwakagenda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Nditiye
Mawaziri na manaibu waziri wakiuaga mwili wa marehemu Nditiye
Post a Comment