Featured

    Featured Posts

WANAOISHI PEMBEZONI MWA VYANZO VYA KUFUA UMEME WA MAJI MTERA, KIDATU WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI +video



Maji yakiwa yamejaa katika kituo cha kufua umeme cha Mtera mpakani mwa mikoa ya Dodoma na Iringa.
Daraja linalokatiza Mtera

Meneja Uhusiano TANESCO, Johary Kachwamba akitoa wito kwa wananchi wa pembezoni mwa mkondo wa maji yatokayo  kituo cha Mtera na Kidatu kuchukua tahadhali ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea wakati wa tukio  la kuyaruhusu maji kupita kwenye mkondo wake wa asili. 


Meneja wa kituo cha kufua umeme Mtera, Mhandisi Elias Mwalupilo akielezea jinsi maji yanavyozidi kuongezeka katika kituo cha kufua umeme cha Mtera hivyo kupanga jinsi ya kuyapunguza kwa kuyafungulia ili yasilete athari za uzalishaji kwenye kituo hicho.


Na Mwandishi Wetu, Mtera

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limewataka wananchi wanaoishi au kuendesha shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mkondo wa maji yatokayo katika mabwawa ya kufua umeme ya Mtera na Kidatu kuchukua tahadhari kutokana na kina cha maji kuzidi kuongezeka. 


Tahadhari hiyo imetolewa na Meneja wa kituo cha kufua umeme Mtera, Mhandisi Elias Mwalupilo, kufuatia maji kuendelea kuingia  kwa mita za ujazo kati ya 600 hadi 1000 kwa sekunde hivyo kina cha maji kuzidi kuongezeka.


"Kina cha maji kinazidi kuongezeka, hivyo inatulazimu hapo baadaye kama hali itaendelea hivi kupunguza maji yaliyozidi kwa kuruhusu kupita kwenye mkondo wake wa asili kwa ajili ya usalama wa miundombinu ya umeme pamoja na daraja" amesema Mhandisi Mwalupilo.


Shirika linalazimika kuyapunguza maji yaliyozidi kina cha juu cha bwawa ambacho ni 698.50 kwa ajili ya usalama wa bwawa na mitambo ya kufua umeme ili iendelee kufanya kazi kwa ufanisi.


Mhandisi Mwalupilo amesema kutokana na mvua nyingi ambazo zilinyesha mwaka jana hasa Nyanda za Juu Kusini Mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe ambako kuna vyanzo vingi vya maji ilipelekea bwawa la Mtera kupata maji mengi, hivyo uwepo wa mvua za wastani mwaka huu kumepelekea kina cha maji katika bwawa la Mtera kuongezeka.


Amevitaji Vijiji vinavyotakiwa kuchukua tahadhari kwa upande wa mkondo wa Mtera ni Keseke, Idodoma wilayani Mpwapwa. Kwa Kilolo ni Nyanzwa na Ruaha Mbuyuni na Wilaya ya Kilosa ni Malolo, Msosa na Kidai A na B.


Mhandisi Mwalupilo aliongeza kuwa Vijiji vinavyotakiwa kuchukua tahadhari kwa upande wa bwawa la Kidatu Wilaya ya Kilosa ni Vidunda, Ruaha, Lyahira na Kitete na Vijiji vilivyopo Kilombero  ni Nyange, Msolwa station na viwanda vya sukari Kilombero.


Kwa upande wake Meneja Uhusiano TANESCO, Johary Kachwamba ametoa wito kwa wananchi hao wa pembezoni kuchukua tahadhali ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea wakati wa zoezi la kuyaruhusu maji kupita kwenye mkondo wake wa asili. 


Amesema TANESCO itaendelea kutoa elimu kwa Wananchi hao, lakini pia kushirikiana na viongozi wa Vijiji, Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji pamoja na Maafisa wa Uvuvi kwa kuzingatia jamii kubwa katika Vijiji hivyo inayojishughulisha na kilimo, ufugaji na uvuvi.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana