Featured

    Featured Posts

WAZIRI MKUU WA TUNISIA AWAPIGA KALAMU NYEKUNDU MAWAZIRI 5

Waziri Mkuu wa Tunisia awapiga kalamu nyekundu mawaziri 5

Waziri Mkuu wa Tunisia amewafuta kazi mawaziri watano katika baraza la mawaziri la nchi hiyo na kuwateuwa wengine kushika nyadhifa hizo.

Hichem Machichi jana Jumatatu aliwafuta kazi mawaziri wake watani ambao Januari 26  Bunge liliwapigia  kura ya kuwa na imani nao. Waziri Mkuu wa Tunisia amewateua mawaziri wengine  baada ya kuwapiga kalamu nyekundu mawaziri hao watano. 

Al Mechichi aidha ameeleza kuwa, yuko tayari kuchunguza njia zitakazodhamini ukamilishaji wa mchakato wa kufanyiwa marekebisho baraza la mawaziri ili liweze kutekeleza majukumu yake katika fremu ya katiba ya nchi. 

Rais Kais Saeid  wa Tunisia tarehe 26 mwezi Januari mwaka jana alimpa jukumu Machichi ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani la kuunda serikali mpya nchini humo.  Ni zaidi ya wiki mbili sasa ambapo Tunisia inakabiliwa na mgogoro kufuatia kula kiapo mawaziri wapya 11 katika serikali mpya ya nchi hiyo.  Rais wa Tunisia amekosoa mchakato unaoendelea sasa nchini humo wa kubadilishwa mawaziri.

Rais Saeid Kais wa Tunisia 

Rais wa Tunisia aidha amelalamikia kuteuliwa baadhi ya mawaziri ambao yeye anaamini kuwa wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi na kesi nyingine ambazo zinatishia maslahi ya taifa. Wakati huo huo Rachid Ghanoush Spika wa bunge la Tunisia ameiunga mkono serikali. 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana