Atlas Madale, Dar es Salaam
Wanafunzi wa Atlas Madale jijini Dar es Salaam, wamefanya Uchaguzi wa Rais 2021/2023 na Abubakar Hajj kuchanguliwa kuwa Rais wa Wanafunzi hao, baada ya kuongoza kwa kupata kura 687 sawa na asilimia 54.9 dhidi ya mgombea mwenzake.
Katika uchaguzi huo ambao ulivutia kwa wagombea hao wawili kuonyesha weledi mkubwa hasa wakati wa kujieleza wakiomba kura kwa wanafunzi wenzao, Abubakar alichuana vikali na mgombea mwenzake wa nafasi hiyo ya Urais, Fanny Foster aliyepata kura 544 sawa na asilimia 43.5.
Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 1251, zikiharibika 20 na kura halali kubakia 1231 ambapo kufuatia uchaguzi huo Abubakar alitangazwa kuwa Rais wa Wanafunzi wa Atlas Kampasi ya Madale kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 huku Angel Boniventura akitangazwa kuwa Makamu wa Rais Atlas Madale 2021/2022.
Habari katika Picha๐
Aliyekuwa Mgombea wa Urais Atlas Madale 2021/2023 Abubakar Hajj akiomba kura kwa wajumbe, wakati wa Uchaguzi huo.Mpigakura Kauthar Haji Abuu wa form Six Red akimuuliza swali Abubakar Hajj
Mpigakura akimuuliza swali Abubakar
Mpigakura Rahma Mohammed akimuuliza swali Mgombea Fanny Foster wakati wa uchaguzi huo. Wapigakura ambao ni wanafunzi wa Atlas Madale wakiwa kwenye Uchaguzi huo.
Upigaji kura ukifanyika baada ya Wagombea kuomba Kura
Chini ni 'Video Clip' Abubakar na mwenzake Fanny wakionyesha umahiri wao wakati wakichuana kuomba kura. Tafadhali, Bofya Hapo๐
Post a Comment