Featured

    Featured Posts

BAADA YA KUSIMAMISHWA KAZI NA RAIS SAMIA, MKURUGENZI WA TPA MHANDISI KAKOKO AKAMATWA, ADAIWA KUKUTWA NA DOLA KIBAO ZA MAREKANI NYUMBANI KWAKE.

 

Mhandisi Kakoko

CCM Blog Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko amekamatwa, ikiwa ni siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za ubadhirifu zinazoikabili TPA.


Habari za uhakaika tulizopa zimeeleza kuwa, baada ya agizo la Rais, Makachero wa Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikwenda nyumbani kwa Mhandisi Kakoko jijini Dar es Salaam na kufanya upekuzi  na inaelezwa kuwa katika upekuzi huo makachezo walikuta kiasi kikubwa cha fedha ndipo wakamkamata kwa ajili ya hatua zaidi.


Rais Samia alifanya uamuzi wa  kumsimamisha kazi Kakoko ili kupisha uchunguzi baada ya kupokea Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/2020 ambayo imeonyesha kuwepo ubadhirifu mkubwa bandarini.

 

“Kuna ubadhirifu mkubwa Bandarini naomba TAKUKURU ikafanye kazi, nimeletewa ripoti ya ubadhirifu wa Bilioni 3.6. Imani yangu ni kwamba ndani ya Shirika la Bandari kuna ubadhirifu kama wa sh. Bilioni 3.6, lakini Waziri Mkuu amefanya ukaguzi na waliosimamishwa ni wa chini, nimeomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu uchunguzi uendelee,”amesema Rais Samia.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana