Na Mwandishi Maalum
Mkurugenzi wa Kampuni ya GF Vehicle Assemblers (GFA) Imran Kamali ametembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dk. Maduhu Kazi, kujadili chanagmoto mbalimbali na fursa za uwekezaji nchini Tanzani.
Katika mazungumzo hayo, Imrani alimwambia Mkurugenzi wa TIC kwa Kampuni ya GF kiwanda chake ndicho pekee cha kwanza nchini Tanzania cha kuunganisha magari ambacho sasa kimeanza uunganishaji wa Malori makubwa(Trucks) ambayo alisema yatampunguza gharama ya uagizaji magari ya aina hiyo nje ya nchi.
Alimwambia kuwa hatua hiyo ya kuanza kuunganisha malori makubwa itawezesha kuimarisha na kupandisha bidhaa za hapa nchini kwa kutotumia fedha za kigeni katika kuagiza magari nje ya nchi.
Naye Mkurugenzi wa TIC Dk. Kazi ameipongeza Kampuni ya GF na kuwakaribishs wawekezaji kuiona fursa hiyo na kuichangamkia kwa kuanzisha miradi mingine kwenye eneo hilo kupitia TIC ili kunufaika na vivutio vya kiuwekezaji ambavyo Serikali imeboresha zaidi kwa ajili ya miradi ya aina hii nchini.
Mradi huu wa pekee na wa aina yake umesajiliwa TIC mwezi Februari 2020 na kuanza uzalishaji mwezi Septemba 2021Wilayani Kibaha mkoa wa Pwani ambapo katika mradi huo Watanzania takribani 100 wamepata ajira kwenye awamu ya kwanza ya utekelezaji na kiasi cha dola milioni 2.5 za Kimarekani kimewekezwa.
Mwisho Mkurugenzi wa GF Imran Karmali amesema, anashukuru kwa ushirikiano alioupata na anaoendelea kuupata kutoka kwa viongozi mbali mbali wa serikali katika Kuhakikisha wanafanikiwa . katika kufikika kufanikisha kuanza kwa mradi huo wa utengenezaji wa Malori.
Pia alisema mpaka kukamilika kwa mradi huo kutaongeza soko la ajira kwa Watanzania katika Nyanja tofauti kuanzia mafundi na hata watoa huduma mablimbali watahusika pia watahakikisha wanazalisha magari kwa soko la ndani nannje yanchi pia hasa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Post a Comment