Kikwete ameyasema hayo leo wakati akitoa salamu za rambirambi katika Uwanja wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita, ambako viongozi mbalimbali akiwemo, Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi na wengine wamehudhuria ibada ya mazishi ya kuuaga mwili ya Hayati Rais Dk John Pombe Magufuli.
Akizungumza kwa kutaja yale aliyoshirikiana naye katika utawala wake, Kikwete alisema baada ya kuona juhudi zake katika wizara mbalimbali alichukua majina matano kati ya 38 la kwanza likiwa la hayati Magufuli na kuyafikisha mbele ya Kikao cha Kamati Kuu ambako kulikuwa na mjadala mkali na hatimaye jina la Magufuli kupitishwa.
“Wapo wazee wastaafu wakina mzee Mangula walinifuata na kuniambia vipi fulani usimuweke namwambia nimesikia, majina yale kwa mara ya kwanza niliyatoa kwenye kikao cha maadili ya Chama Cha Mapinduzi, mjadala mkali kweli kwa nini umemuacha fulani, hawa wepesi, hawatoshi,”alisema Kikwete.
Post a Comment