Featured

    Featured Posts

JKT YATANGAZA MKAKATI KABAMBE UZALISHAJI MAZAO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI+video

..

KAIMU Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa jeshi hilo , Kanali Hassan Mabena (pichani) amesema kuwa wamechukua hatua za makusudi katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kutimiza azma ya JKT kujitegemea kwa chakula na pia kuzalisha mazao ya biashara.Akizungumza mwishoni mwa wiki, wakati wa hafla ya Wizara ya Kilimo na JKT kusainiana mkataba wa ushirikiano wa kuboresha sekta ya kilimo, Kanali Mabena amesema kuwa katika kuimarisha uzalishaji kwa tija JKT imenunua matrekta 15 pamoja na zana nyingine za kilimo.Aidha, Kanali Mabena amesema wameanzisha shamba la umwagiliaji la mpunga eneo la Chita wilayani Kilombero, Morogoro ambapo pia wanaanza ufugaji wa samaki, ng'ombe na mifugo mingine.

Mafanikio na Mabadiliko yote hayo makubwa yametokea tangu Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbuge ashike wadhifa huo mwaka 2019, ambapo aliunda kamati hiyo ya kimkakati mahsusi ili malengo yatimie, ya JKT kujitosheleza kwa chakula na ziada kuuza kwa wananchi.

Mdau, naomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Kanali Mabena akielezea kwa kina kuhusu mikakati mbalimbali waliyoipanga kutimiza lengo hilo kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo....
IMEANDALIWA NA: 
RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana