Na Paineto Makweba, Dodoma
Maafisa Ukaguzi wa Mazingira nchini kote wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa mazingira wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Barnabas Ndunguru kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga kwenye hafla ya kuwakabidhi vitambulisho Maafisa Usimamizi 34 waliofaulu mafunzo ya Usimamizi wa Mazingira.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma, Ndunguru amesema suala la usimamizi wa mazingira ni la msingi na muhimu kwa jamii, hivyo sheria, kanuni na taratibu zinapaswa kufuatwa.
“Kwa hivi vitambulisho mnavyokabidhiwa leo, tunaamini mmepata mafunzo ya kutosha kuwawezesha kuwa na weredi wa kusimamia na kutumia busara, sheria na kanuni zinazotakiwa katika usimamizi wa mazingira.”
Aidha, amesisitiza wawe na utamaduni wa kujisomea mara kwa mara sheria za mazingira, Maji na ardhi ili kuendana na mabadiliko ya kanuni.
Mafunzo ya Usimamizi wa Mazingira yameendeshwa na kusimamiwa kwa ushirikiano wa Wizara ya maji na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Barnabas Ndunguru akizungumza na Maafisa ukaguzi (hawapo Ppichani) kabla ya kukabidhiwa vitambulishoPicha ya pamoja ya Maafisa Ukaguzi mwishoni mwa hafla hiyo ya kukabidhiwa vitambulisho vya ukaguzi wa mazingira
Post a Comment