Featured

    Featured Posts

MKUU WA WILAYA YA KYERWA MKOANI KAGERA AAGIZA UHAMIAJI KUCHUNGUZA URAIA WA DIWANI ALIYETOA KAULI CHAFU JUU YA SERIKALI.

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Rashid Mohamed Mwaimu akizunumza jambo wakati wa kikao hicho

Diwani wa kata ya kitwe Benan Laurian Rwabalema aliyetoa kauli zenye kuichafua serikali

Na Lydia Luakila

Kyerwa:-

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Rashid Mohamed Mwaimu ameiagiza idara ya uhamiaji wilayani humo kuchunguza uraia wa diwani wa kata ya kitwe kupitia chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema Benan Laurian Rwabalema baada ya kutoa kauli zenye kuichafua serikali huku mwenyekiti wa Halmashauri hiyo akimtaka diwani huyo kuleta vielelezo vya uthibitisho juu ya tume ya uchaguzi wilayani humo kuruhusu vitendo vya uvujifu wa Sheria za uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka 2020 kwa kuruhusu kutapakaa kwa karatasi za kupigia kura  mitaani.


Hayo yameibuka katika Kikao cha baraza la madiwani cha halmashauri hiyo.


Baraza hilo chini ya mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Bahati Enerco diwani huyo wa kata ya kitwe Benan Laurian Rwabalema alihoji masuala ya mapato na matumizi na kusema mh, mwenyekiti ukiachilia nguvu kubwa zinazowekwa katika kuimalisha mapato yetu lazima tuweke nguvu ile ile katika matumizi ambapo Kuna fedha imetengwa kwa ajili ya kufanya uchaguzi mdogo lakini mhe. mwenyekiti utakubaliana na mimi kwamba tume ya uchaguzi imekuwa ikiruhusu vitendo vya uvujifu wa Sheria za uchaguzi nna hivyo kuichafua sura na taswira ya kidemokrasia katika nchi yetu ambapo tume hii iliyoruhusu karatasi za kupigia kura kutapakaa mitaani hasa katika kata yangu alisema diwani huyo"


Baada ya hatua hiyo ndipo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo alimtaka diwani huyo kuthibisha kauli hiyo kisha diwani huyo kushindwa kuithibitisha huku akikiri kwamba hana uthibitisho jambo lililomfanya mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Rashid Mohamed Mwaimu kuiagiza idara ya uhamiaji wilayani humo kuchunguza uraia wa diwani huyo kwani amekuwa akitoa kauli zenye kuichafua serikali ambapo kwa mujibu wa viongozi wilayani humo ni mara ya pili kufanya kitendo hicho ambapo Mara ya kwanza alizuiliwa kuhudhuria mkutano wa kwanza kutokana na kauli zake.


Mkuu wa wilaya hiyo Rashid Mwaimu amesema kuwa uchaguzi umeisha sio muda wa viongozi kuleta marumbano na maneno yasiyojenga badala yake wanatakiwa waachane na maneno wakawahudumie wananchi waliowachagua.


"haiwezekani kuichafua na kuipaka matope serikali sitakubali nitapambana na watu wa namna hii kama wewe ni pandikizi tutakushughulikia nataka  vielelezo ulivyoagizwa na mwenyekiti juu ya uthibitisho vipitie kwangu   huku akiahidi kupambana na viongozi wa namna ile wanaokwenda kinyume na taratibu.


Amewataka viongozi wilayani humo kufuata Sheria kanuni na taratibu katika kudai haki bila kuikashfu nchi wala kuzua taharuki kwa wananchi.


Kwa upande wake afisa uchaguzi wilayani humo amekemea kauli ya diwani huyo yenye upotoshaji na kuwa  uchaguzi huo ulifanyika kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na tume ambapo haki pia ilitendeka.


Hata hivyo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amewataka madiwani hao kutumia busara katika kutoa hoja na kisha kutoa siku tatu diwani huyo kuleta uthibitisho unaonyesha kutapakaa kwa karatasi za kupigia kura mtaani kwake.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana