Featured

    Featured Posts

MTAALAM TMDA AZUNGUMZIA UBORA WA VITAKASA MIKONO (SANITIZER)

 


Mchunguzi wa Dawa na Bidhaa za Nyongeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Gerald Sambu akiwaelezea waandishi wa habari hawapo pichani namna wanavyopima ubora wa vipukusi katika maabara hiyo.

Mchunguzi wa Dawa na Bidhaa za Nyongeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Gerald Sambu akiwaelezea waandishi wa habari mashine mbalimbali zilizopo kwenye maabara hiyo zinazotumika kupima ubora wa vipukusi na bidhaa nyingine katika maabara hiyo.

Hii ni Mashine ya HPLC inayotumika pia kupima ubora wa dawa mbalimbali katika maabara hiyo.

Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba  (TMDA)Gaudensia Simwanza akifafanua jambo kwa waandishi wa habari waliotembelea katika maabara hiyo kwa ziara ya kimafunzo.

………………………………………….

Vipukusi(Sanitizer) ambavyo vipo kwenye hali ya kiminika na Vinavyoweza kukauka ndani ya sekunde 30 au dakika 1,ndivyo vyenye ubora zaidi kwa matumizi katika mikono yako kwa sababu vina uwezo wa kuua haraka vijidududu kuliko vilivyo katika hali ya mnato ambavyo vinaweza kubeba vijidudu mikononi mwako na kusababisha maambukizi.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea maabara ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Mabibo mkoani Dar es salaam. Mchunguzi wa Dawa na Bidhaa za Nyongeza katika maabara ya TMDA Bw. Gerald Sambu amesema Vitakasa mikono (Sanitizer) vilivyo katika hali ya kimiminika ni bora zaidi kwa sababu unapotumia katika mwili ngozi yako inakauka na vinakuwa na uwezo mzuri wa kuua vijidudu mbalimbali kutokana na kuwa na kiwango cha kutosha cha kemikali inayofanya kazi hiyo.

“Utendaji wa kemikali kwenye hali ya kimiminika unakuwa mzuri zaidi kuliko ile iliyokuwa nzito na mafuta yaani (Gel),ufanisi wake unakuwa si mzuri kwa sababu unakuwa na vitu vingine vilivyombatana na kemikali hivyo kushindwa kuua vijidudu kwa wakati,” Amesema Sambu

Ameongeza kuwa kipukusi kikiwa katika hali ya kimiminika ni bora zaidi kwa sababu kina uwezo wa kuua (Bakteria) na vijidudu mbalimbali jambo muhimu kiwe na kiwango cha kutosha cha kilevi (Alcohol) cha wastani wa asilimia 70 kama inavyoshauriwa na Shirika la Afya Duniani WHO.

Kwa mwananchi wa kawaida anaweza kubaini kipukusi chenye ubora kwa kuangalia kama kimesajiliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) au kwa kuangalia  tarehe ya kuharibika (Expire Date) wakati anapoinunua kwenye maduka ya dawa.

Naye Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba  (TMDA)Gaudensia Simwanza amesema mbali na uchunguzi huo wa Kisayansi na kimaabara unaofaywa ili kudhibiti ubora wa dawa na vifaa tiba Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba imekuwa ikifanya ukaguzi mbalimbali kwa kutimia wakaguzi wake  katika maeneo kama Bandarini,Viwandani na katika maduka ili kubaini kama kuna bidhaa yoyote imeingizwa au kuzalisha bila kufuata utaratibu wa ubora na udhibiti wa dawa na vifaa tiba.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana