Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUCTA, Rehema Ludanga akizungumza maneno ya utangulizi wakati wa kongamano hilo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. |
Washiriki wakiimba nyimbo za hamasa.
Mkurugenzi wa Wanawake na Vijana wa Tucta, Siham Ahmed akizungumza maneno ya utangulizi.
Katibu Mkuu wa Tucta, Said Wamba.
Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya.
Mwakilishi wa Chama cha Waajiri Tganzania (ATE), Anabahati Mlay.
Naibu Ktibu Mkuu TUGHE, Jane Mbura akito neno la shukrani kwa mgeni rasmi, Naibu Waziri Ummy.
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Rehema Ludanga amesema Mwanamke ambaye ni kiongozi lakini hawezi kumuinua mwanamke mwenzie kimaendeleo ana nafasi yake kuzimu.
Maneno hayo machungu ameyazungumza wakati wa Kongamano la wiki ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani lililofunguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Ummy Nderiananga jijini Dodoma Machi 7, 2021.
"KUNA nafasi yake kuzimu Mwanamke kiongozi ambaye ana nafasi ya kuwasaidia wanawake wenzie na hafanyi hivyo. Nafasi ya uongozi uliyoipata usiione kuwa ni ya kwako peke yako, ni ya wanawake wote,"amesema Rehema.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Rehema Luganga akiwapa somo hilo, lakini vile vile Rais wa Tukta, Tumaini Nyamhokya na Naibu Waziri Ummy Nderiananga wakihutubia wakati wa kongamano hilo ambalo pia iliendeshwa mada ya hatua muhimu za kujikinga na kukabiliana na janga la Corona mahala pa kazi...
Post a Comment