Featured

    Featured Posts

NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AIPONGEZA TAKUKURU KWA KAZI NZURI YA KUTOKOMEZA RUSHWA NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Brigedia Jenerali John Mbungo akimkabidhi Naibu Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi nyaraka ambazo ni vitendea kazi vyao wakati wa Mkutano Mkuu wa Viongozi wa Taasisi hiyo nchini, uliofanyika jijini Dodoma jana Machi 2, 2021. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Sehemu ya viongozi wa Takukuru kutoka mikoa yote nchini wakisikiliza wakati Naibu Waziri Ndejembi akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali Mbungo akielezea mikakati mbalimbali ya kupambana na Rushwa nchini na mafanikio waliyoyapata. ndani ya miaka mitano ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Naibu Waziri Ndejembi, akihutubia katika mkutano huo ambapo ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri yenye mafanikio makubwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa wa Takukuru, Sabina Seja akitoa shukrani na kuahidi yote waliyoelekezwa na Naibu Waziri, Ndejembi watayafanyia kazi.
Naibu Waziri Ndejembi akionesha zawadi aliyozawadiwa na Takukuru.
Naibu Waziri Ndejembi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Mahenge na Mkurugenzi wa Takukuru akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo.



Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ndejembi  akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge (kushoto) baada ya Ndejembi kufungua Mkutano Mkuu wa Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini  (Takukuru), uliofanyika jijini Dodoma leo Machi 2,2021. Katikati ni  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali Mbungo akimpigia saluti Naibu Waziri, Ndejembi alipokuwa akimuaga.
Naibu Waziri Ndejembi akibadilishan mawazo na  viongozi mbalimbali walihudhuria mkutano huo. Kutoka kushoto ni; Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali Mbungo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Mahenge.

 Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali Mbungo (kulia) akijadiliana jambo na  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy (kushoto)  na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma,  Kibwengo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana