Na Mwandishi Maalum, Njombe
Waziri Mkuu wa Kassim Majaliwa amesema Rais Dk. John Magufuli yupo salama na anaendelea na majukumu yake kama kawaida na kuwataka Watanzania kuwapuuza wapotoshaji wanaosambaza taarifa za chuki, uongo na kuzua taharuki miongoni mwa wanajamii kuhusiana na afya ya Rais.
Waziri Mkuu amesema hayo, leo baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Njombe, na kussema kuwa tabia ya baadhi ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi ya kupotosha makusudi mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi pamoja na Kuzusha Uongo ni tabia ya hatari ambayo inalenga kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuzusha taharuki katika jamii.
"kwa hili na mimi Nionyeshe Masikitiko yangu kwa wanaosambaza uzushi juu ya afya ya Kiongozi wetu na kuleta taharuki kuwa rais wetu anaumwa jambo ambalo ni uongo kwani mimi asubuhi nilizungumza naye nikamfahamisha juu ya ziara yangu mkoani Ruvuma" aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa
"Rais ana mambo mengi na kutoka kwake ni kwa ratiba ya mpango kazi wake, unataka rais atoke aanze kuzurura Kariakoo, au aanze kuzurura Magomeni, au unataka azunguke kwa ratiba yako?" aliongeza Majaliwa
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Watanzania kuwaombea Viongozi Wakuu wa nchi kwani wana Dhamana kubwa ambayo wamepewa ya kuwatumikia.
Post a Comment