Zuio hilo linaanza kutekelezwaaa sita usiku wa Ijumaa .
Kaunti nyingine zilioathiriwana azui hilo ni Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru .
Hakuna usafiri wa barabarani ,angani na reli utakaoruhusiwa kuingia na kutoka sehemu hizo zilizotajwa kama zenye janga 'zilizoathiriwa sana na Corona'.
Maeneo hayo yatakuwa chini ya masharti hayo ya zuio kwa siku 30 zijazo .
Baada ya kuwahutubia Wakenya Rais Uhuru aliwaongoza maafisa wakuu wa serikali kupokea chanjo ya corona katika Ikulu ya Nairobi.
Baada ya kutangaza masharti mapya ya kupambana na ongezeko la visa vya Covid 19 nchini Kenya rais alikuwa wa kwanza kuchanjwa kisha mkewe Margaret Kenyatta akachomwa chanjo hiyo .
Wengine waliochanjwa ni waziri wa usalama wa Ndani Fred Matiang'i , Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, waziri wa mashauri ya kigeni Raychelle Omamo ,Kaimu Jaji mkuu Philomena Mwilu na viongozi mbalimbali wakiwemo wa kidini .
Rais amewasisitiza Wakenya wachanjwe dhidi ya virusi hivyo baada ya serikali kutangaza kwamba itawapa kipaumbele watiu walio na umri wa miaka 58 na zaidi katika kutoa chanjo hiyo .
" Ukiwapima Corona Wakenya 100 ,watapatikna 20 na virusi hivyo.
Kiwango cha maambukizi kimezidi mara kumi zaidi' rais Kenyatta amesema
Uhuru amesema wimbo la tatu la janga ilo nchini Kenya linatarajiwa kufika kilele chake katika siku 30 zijazo .
Akilihutubia taifa siku ya ijumaa rais Kenyatta pia alifanyia mageuzi marufuku ya kutotoka nje ambapo sasa marufuku hiyo itaanza saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri katika kaunti hizo tano ilhali itaendelea kuanza saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri katika sehemu nyingine za taifa .
Masharti mengine ni yapi?
Kando na kuzuia usafiri wa watu katika kaunti hizo tano rais enyatta pia amepiga marufuku mikutano au mikusnayko ya watu katika maeneo hayo.
Bunge nalo pia limechukua pamojana mabunge ya kaunti zilizotajwa hao juu.
Serikali pia imefutoilia mbali pasi zilizokuwa zimetolewa kwa watu wanaotoahuduma muhimu kwani zimekuwa zikitumiwa vibaya na wizara ya Afya na ile ya usalama wa ndani zitatathmini upya mwongozo wa kuzitoa pasi hizo.
Shughuli zote zakuabudu katika kaunti za Nairobi, Nakuru, Machakos, Kiambu, na Kajiado zimezuia hadi wakati uamuzi huo utakapobadilishwa .
Katika hatua ambayo huenda tena ikawahamakisha wafanyibiashara katika sekta ya burudani ,baa hazitaruhusiwa kuhudumu katika kaunti hizo tano husika na mikaha imetakiwa kutoa huduma za kuwapelekea wateja vyakula waliko na imepigw amarufuku dhidi ya kuuza pombe
Hakuna masomo ya ana kwa ana yatakayokubaliwa na vyuo viku vyote na shule zimefungwa . Wafanyikazi wa mashirika ya serikali na ya kibinafsi wametakiwa kufanyia kazi nyumbani isipokuwa kwa wale wanaotekeleza uduma muhimu zinazowahiaji kwenda kazini. Hospitali zimetakiwa kupunguza idadi ya watu wanaokuja kuwaona wagonjwa hadi mtu mmoja kwa kila mgonjwa .
Mikutano yoteitakayoruhusiwa itakuwa na watu wasiozidi 50 ilhali mazishi yataandaliwa ndani ya kipindi cha saa 72 na ni watu 50 pekee watakaoruhisiwa mazishini .
Serikali pia imesema watu walio na umri wamiaka 58 na zaidi ndio watakaokuwa wa kwanza kuchanjwa .
Usafiri kutoka Nje ya Kenya
Kuhusu usafiri wa kigeni Kenyatta amesema safari zote za kimataifa zitaendelea ingawaje cini ya masharti makali ya kuzuia kusambaa kwa Corona .
Amesema wageni wanaoingia Kenya watahitajika kuwana vyeti malaum vya kuthibitisha kwamba wamepimwa corona na hawana virusi hivyo.
Vipimo hivyo vinafaa kufanywa saa 96 kabla ya kuwasili Kenya .
Kenya ilikuwa imelgeza masharti hayo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kupungua kwa visa vya maambukizi lakini idadi ya maamukizi ya ugonjwa huo imekuwa ikiongezeka katika wiki za hivi karibuni .
Nairobi imetajwa kusheheni asilimia 60 ya visa vyote vya maambukizi ya Corona vinavyosajiliwa nchini Kenya
Post a Comment