Featured

    Featured Posts

SERIKALI YAVUKA LENGO UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA 2,257 YAJENGWA

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,akitoa taarifa maalum ya utekelezaji kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo March 2,2021 jijini Dodoma

………………………………………………………………………………….

Na Alex Sonna, Dodoma

SERIKALI imevuka lengo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya kuchukua wanafunzi 74, 166 wenye sifa za kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021 ambao hawakupangiwa shule katika awamu ya kwanza.

Mahitaji ya vyumba hivyo yalikuwa 1,484 na vilivyojengwa ni 2,257  ndani ya miezi miwili ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa Desemba mwaka jana, kwa Wakuu wa Mikoa ambapo aliwataka kuhakikisha wanafunzi wenye sifa za kujiunga na kidato cha kwanza ambao hawakupangiwa shule katika awamu ya kwanza  wanapata nafasi ifikapo Februrai 28 mwaka huu.

Akitoa taarifa maalum ya utekelezaji wa agizo hilo leo March 2,2021 jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, amepongeza Wakuu wa Mikoa kwa ufanikisha ujenzi huo ambapo kwasasa kuna ziada ya madarasa 773.

“Tungeweza kuchukua wanafunzi wengine kwa ziada ya vyumba hivyo tungekuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 38,684,”amesema.

Ameagiza Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuanza kufanya maoteo ya wanafunzi watakajiunga na elimu ya awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 na maandalizi ya miundombinu na madawati kuanza mara moja.

Pia Jafo amesema Serikali ilishatoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya shule za sekondari na kutaka miundombinu hiyo ikamilike kabla ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano 2021 utakaofanyika mwezi Mei, mwaka huu.

Amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa, kuhakikisha ujenzi wa mabweni, madarasa, maabara , ujenzi wa matundu vya vyoo unakamilika haraka.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana