Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti katika shule ya Ndurugumi wilayani Kongwa, Dodoma Machi 12,2021.
Ndugai akizungumza na baadhi ya maofisa wa SBL pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari Development, Bernard James (wa tatu kushoto).
Ndugai akizungumza wakati wa shughuli ya upandaji miti. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Ocitti.
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Ocitti akipanda mti katika shule ya sekondari Mang'weta.
Ndugai amaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa akifurahi baada shughuli ya kupanda miti katika shule ya Mang'weta kukamilika.
Kikundi cha ngoma kikiburudhisha baada ya kupanda miti Laikala
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Habari Development, James akizungumza kuhamasisha upandaji miti wilayani Kongwa.
Wananchi wakielea jinsi walivyo furahishwa na zoezi hilo la upandaji miti
Spika Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL
Spika Ndugai akiwa na baadhi ya walimu wa shule ya Laikala
Wananchi wakishiriki kupanda miti
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti wameongoza shughuli ya upandaji miti 3000 katika shule tatu za sekondari wilayani Kongwa, Dodoma leo Machi 12,2021.Zoezi hilo la upandaji miti katika shule za sekondari Mang'weta, Laikala na Ndurugumi umeratibiwa na Tasisi ya Habari Development na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Akizungumza wakati wa upandaji miti hiyo ambao pia uliwashirikisha kiasi kikubwa wananchi wa maeneo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti amesema kuwa upandaji miti wilayani Kongwa ni sehemu ya mkakati endelevu wa SBL unaolenga kupanda miti sehemu mbalimbali nchini.
"SBL inachukua miti kama sehemu ya mazingira. Miti inasidia uhifadhi wa vyanzo vya maji, ni makazi kwa wanyama na wadudu,inavuta hewa chafu ya kaboni na kuzalisha hewa safi, lakini piaa ni chanzo cha dawa. Biashara yetu na jamii kwa ujumla ni sehemu ya mazingira na hii inatufanya kuwa jukumu letu sote kuyalinda na kuatunza,"amesema Ocitti.
Kwa upande wake Spika Job Ndugai amaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, ameishuru SBL kwa kuunga mkono juhudi za upandaji miti na kuongeza kuwa miti ina nafasi pekee kwa maisha ya watuna kusisitiza kuwa bila miti hakuna maisha.
Ndugai, amesema kuwa ukataji miti holela ni moja kati ya sababu za mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamesababisha changamoto nyingi zinazomkabili binadamu ikiwa ni pamoja na athari kwenye uzalishaji wa chakula, upatikanaji wa maji, afya ya viumbe mbalimbali ikiwa pamoja na binadamu.
"Ni matumaini yangu kwamba zoezi hili la upandaji miti litawavuta wakazi wengi wa Kongwa na wananchi wa maeneo mengine nchini kupanda miti kila wanapopata fursa. Pia napenda kuzikumbusha taasisi na kampuni kufikiria juu ya dunia yetu nakuchukua hatua za kuilinda na kuitunza," amesema Spika Ndugai.
Ndugai amemalizia kwa kuipongeza Taasisi ya Habari Development ka juhudi zake kubwa za kupanda miti kwa lengo la kuigeuza Dodoma kuwa ya kijani.
Post a Comment