Featured

    Featured Posts

WAMACHINGA, BODABODA WAMLILIA RAIS HAYATI DKT MAGUFULI WASEMA ALIWATENGENEZEA MAZINGIRA YA KUFANYA KAZI ZAO BILA USUMBUFU

 


Mwenyekiti wa umoja wa wa machinga mkoa wa Arusha Amina Njoka
mwenyekiti wa madereva bodaboda  mkoa wa Arusha Godlight Rugemalila.
*********************************************
NA  NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Viongozi wa umoja wa wamachinga na umoja wa madereva wa bodaboda mkoa wa Arusha wamesema wamepata pigo na mshtuko mkubwa baada ya kusikia taarafa za kifo za aliyekuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Magufuli kwani hawakulitegemea jambo hilo.
Wamesema Rais Hayati Magufuli aliwatengenezea mazingira bora ya kufanya kazi pamoja na kuwaondolea adha ya kufukuzwa na kukamatwa na Mgambo.
Mwenyekiti wa umoja wa wamachinga mkoa wa Arusha Amina Njoka alisema kuwa wamepeta hofu lakini mwenyezi Mungu awasamehe kwani ni upendo wake aliouchagua kwasababu wao kama wanadamu walipenda kumuona akiishi.
Alisema kwa niaba ya wamachinga  mkoa wa Arusha wamepata pigo kubwa sana kwani aliwafanyia mambo makubwa lakini wanajipa moyo na kumuomba Mungu ayabariki yale aliyowaachia yasije yakabadilika kwani  tegemezi lao lipo ndani ya watanzania.
“Sisi tulikuwa tunamwamini, tulimkubali na kumuheshimu kwasababu alituheshimu na kututoa kwenye mateso makubwa ya kukimbizwa na kukamatwa na mgambo ambao ulikuwa ni utumwa, akatuondolea na kutuweka katika amani na uhuru wa kufanya biashara mahali popote tunapopataka,” Alisema Amina Njoka.
Alifafanua kuwa mpaka dakika hii wamachinga wengi wamepata maendeleo kutoka na mambo mengi aliyowafanyia Hayati Rais Dkt Magufuli ikiwa ni pamoja na watoto wao kupata elimu bure na huduma za afya kuwa karibu nao.
“Ukweli ametufanyia mengi lakini nashindwa kuongea sana tulikuwa tunampenda lakini mwenyezi Mungu kampenda zaidi, Mungu atusaidie watanzania wote tupate ujasiri kumuangalia Mungu atatupa kipi chema mbele yetu,” Alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa madereva bodaboda  Godlight Rugemalila alisema kuwa wamejisikia vibaya sana kwani hayati Rais Dkt Magufuli amewatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao kwa kuwatengenezea miundo mbinu ya barabara lakini pia kuwafanya watambulike.
“Ametufanya tuweze kufanya kazi kwa pamoja, tunasikitika kutokea kwa kifo chake lakini tunaomba viongozi waliobaki waweze kuendeleza yale yoye aliyoyaanzisha ili tisije kujuta kwani Mungu ana makusudi yake,”Alisema Godlight.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana