Msafara wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika barabara ya Airport kuelekea katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya shughuli za kuagwa na maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani leo tarehe 24 Machi 2021.
………………………………………………………………………………………
· Wananchi baadhi wapoteza fahamu
· Biashara zafungwa
· Akina mama watandika khanga na mashuka
· Mkolani wazuia msafara wake
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
Maelfu ya waombolezaji hao wa Mwanza wakiwemo kutoka mikoa jirani ya Mara, Simiyu, Shinyanga walifurika kwenye uwanja huo mapema tangu majira ya sa 9:00 usiku huku baadhi yao wakilala na wengine kukesha uwanjani hapo.
Wakizungumza jana jijini hapa kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walisema kifo cha Rais John Magufuli ni pigo kwa taifa na kumtaja kiongozi kuwa kiunganishi cha Watanzania kwa maendeleo.
Ris huyo wa Awamu ya tano alifariki Machi 17, mwaka huu katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.
Walisema alikuwa kiongozi aliyekuza uchumi wa nchi na kuwezesha Watanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sera ya viwanda na alihimiza uwajibikaji ana kuwataka wananchi kuchapa kazi kwa bidii.
Walisema Rais Dk. Magufuli alikuwa kunganishi cha wananchi wanyonye na Watanzania wote kwa maendeleo ambapo aliwezesha kufufuliwa kwa reli na kujenga ya kiwango cha Kimataifa,meli mpya na kukarabati myingine,Bwawa la kufua umeme la Nyerere na kunganisha mikoa na wilaya kwa barabara za lami.
Walisema kiongozi huyo huyo alitaka kuiona Tanzania inakuwa sawa na Ulaya kutokana na utajiri wa rasilimali zake nyingi yakiwemo madini ambapo alilenga rasilimali hizo ziwanufaishe wananchi wanyonge huku akipinga Tanzania kuitwa maskini ilhali ikiwa na utajiri lukuki.
Wananchi hao mkoani Mwanza waliiambia kuwa,watamkumbuka Hayati Rais Magufuli kwa mambo mengi mazuri aliyowafanyia ikiwemo utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo yote ikigusa maisha ya watu ya kila siku ikilenga kukuza uchumi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA),Mhandisi Leonard Msenyele, alisema atahakikisha anaitekeleza miradi yote ya maji jijini humu iliyoanzishwa na Rais Magufuli, kwa wakati.
Alisema kwa dhati ya moyo wake ili kuenzi alama ya uongozi uliotukuka wa kiongozi huyo wa awamu ya tano ni kutekeleza kwa vitendo mazuri aliyofanya enzi za uhai wake akiaamini pia wananchi wa Mwanza watamkumbuka kwa miradi ya maji.
Mkazi wa Buhongwa Pili Joseph alisema Watanzania hasa wananchi masikini,watamkumbuka Hayati Rais Magufuli kwa mengi na alikuwa kimbilio lao hivyo ni dhahiri kifo chake ni pengo kubwa na pigo mno kwa taifa.
Alisema wananchi wa hali chini na maskini walipata faraja kwa kauli na matendo yake na kuponya mionyo iliyopondeka ambapo aliwezesha waliodhulumiwa kupata haki zao.
Mkazi wa Kijiji cha Bulamba,wilayani Ukerewe,Kawawa Costantine, alisema Magufuli alikuwa mtu wa kazi,mwenye msimamo usioyumba,aliwapenda wananchi wake na alidhihirisha hilo alipoamua kushughulikia kero na kutatua matatizo ya watu wa hali ya chini,hivyo wataendelea kumbukuka kwenye mioyo yao.
“Ni Rais aliyekuwa na maono ya pekee,hakutaka kuiona Tanzania nchi yenye utajiri wa madini kila aina ikiitwa masikini,alipambana na ufisadi na ubadhirifu bila woga,aliwahi kusema maisha yake ameyatoa sadaka kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania masikini na kuomba tumwombee sababu si wote waliokuwa wakifurahia na kumpenda kwani alijitoa kwa wanyonge,”alisema Kawawa.
Aidha, Mkazi wa Kijiji cha Kamanda Stella John alisema Hayati Rais Magufuli, aliwagusa wanawake wajane na kuhakikisha wanapata haki na fursa za uongozi hata kwenye kujifungua amewaboreshea wanapata huduma bora za afya ya uzazi,aliwawezesha mikopo wanawake wajasiriamali,vijana na walemevu.
Pia walisema kitendo cha kuamua kutoa elimu bure kwa shule ya awali hadi kidato cha nne,kulirejesha matumaini ya kupata elimu kwa watoto wa masikini, hivyo wengi watakumbukwa kwa kuboresha elimu na huduma mbalimbali za kijamii.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa,kiuchumi na kijamii walisema ni kiongozi aliyekuwa na maono,jasiri aliyethubutu na asiyependa kukwamishwa kwa jambo analotaka liwe.
Alijenga imani kubwa kwa Watanzania wa kada mbalimbali kutokana na miradi mingi ya kimkakati iliyolenga kukuza uchumi na kutatua kero za wananchi, hivyo itachukua muda mrefu kuondoka kwenye mioyo ya Watanzania.
Post a Comment