Featured

    Featured Posts

DAWASA: WANAOHUDUMIWA NA RUVU JUU KUKOSA MAJI LEO KUTOKANA NA MATENGENEZO MTAMBONI


DAWASA, Dar es Salaam

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi wanaohudumiwa na Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji leo tarehe 8/ 4/2021.


Taarifa iliyotolewa leo Aprili 8, 2021 na Kitengo cha Mawasiliano na Jamii cha DAWASA imetaja maeneo yatakayoathirika kuwa ni  Mlandizi, Ruvu Darajani, Vikurutu, Visiga, Misugusugu, Kongowe, Soga, Maili 35, Kwa Mfipa, Mwenda Polepole, Kwa Mathias, Mkuza, Picha ya Ndege na Shirika la Elimu Kibaha.


Maeneo mengine ni, Pangani, Maili Moja, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Temboni, Kwa Msuguri, Saranga, Golani, Stop Over, Bonyokwa, Changanyikeni, Buguruni, Ubungo, Kisiwani, Msewe, Kilungule, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kiwalani, Pepsi hadi  Airport.


Taarifa hiyo imesema sababu ya ukosefu wa majisafi ni hitilafu  kwenye mfumo wa umeme mtamboni na kwamba jitihada za kutatua tatizo hilo zinaendelea.

 

"Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. Kwa taarifa zaidi, wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja  0800110064 au *152*00# (BURE)", imekamilisha taarifa hiyo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana