Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo leo jioni, Aprili 30, 2021 ameripoti Ofisini na kuendesha kikao maalum cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma, jijini Dodoma.
Pamoja na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Kikao hicho kimehudhuriwa na Wajumbe wapya akiwemo Naibu Katibu Mkuu - Bara Christina Mndeme na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.
Kikao hiko maalum cha utambulisho, pia kimejumuisha viongozi wastaafu wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara Rodrick Mpogolo na aliyekuwa Katibu wa NEC, Oganaizesheni Pereira Ame Silima.
Katibu Mkuu Chongolo, ameripoti ofisini baada ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kumpitisha leo na pia kupitisha Makatibu NEC wa Idara za CCM baada ya majina yao kuwasilishwa kwenye Kikao hicho na Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akishuhudia wakati Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdallah Juma Mabodi wakati aliporipoti Ofisini na kuendesha kikao maalum cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma, jijini Dodoma, leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka. Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiendesha kikao hicho.
Post a Comment