Featured

    Featured Posts

MBUNGE JIMBO LA TEMEKE MHE.DOROTHY KILAVE GEORGE AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA CRDB TAWI LA TEMEKE.

LEO April 06, 2021.
Mhe. Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave  akizungumza jambo na baadhi ya Viongozi wa CRDB (pichani hawapo) ambapo Kikao hicho kilifanyika muda wa Saa 4:30 Asubuhi Maeneo ya Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo.

Lengo lakikao hicho ni kufanya Mazungumzo na Benki ya CRDB juu ya kutoa Mikopo ya Riba Nafuu Pamoja na Elimu ya Usimamizi wa Fedha kwa Wananchi wa Jimbo la lake.

Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe Dorothy Kilave George amewaeleza Maafisa hao juu ya namna serikali inavyotoa Mikopo kupitia Manispaa zetu lakini  amedhamiria kupanua wigo wa Mikopo katika makundi matatu (*Walemavu,*Kinamama na *Vijana) 

Mr. Endrew Augustine ambaye ni Manager wa Tawi la CRDB Temeke Amekubaliana na Maombi ya Mhe. Mbunge wa Jimbo la Temeke na ameahidi kuandaa utaratibu maalumu kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa Temeke kwa Mikopo ya Riba nafuu  Pia watashiriki kwa ukaribu sana kuhakikisha wanatoa mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa Vikundi na wajasiriamali Kama ilivyokubaliwa.

Kutoka 
Ofisi ya Mbunge Jimbo  la Temeke.
06/04/2021.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana