MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Mhe. Neema Lugangira akichangia kwenye Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo alijiwekeza kwenye mambo mawili ya Lishe na Sekta ya Asasi za Kiraia (NGOs, CSOs na CBOs)
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Mhe. Neema Lugangira ameiomba Serikali iikaribishe Sekta ya Asasi za Kiraia kama ilivyowakaribisha Sekta Binafsi kutokana na utayari wao kushirikiana na Serikali .
Aliyasema hayo leo wakati akichangia kwenye Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo alijiwekeza kwenye mambo mawili ya Lishe na Sekta ya Asasi za Kiraia (NGOs, CSOs na CBOs) ambapo alisema awali alikuwa na hofu juu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kumezwa na Afya.
Hata hivyo alisema anamshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulitambua hili na kuweka naibu waziri anayesimamia Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto hatua ambayo itakuwa chachu ya kufanikisha Mipango ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Mhe Neema Lugangira alisema pia Sekta ya Asasi za Kiraia ina mchango mkubwa kwa sababu inaajiri watu wengi sana na kwa Taarifa ya Wizara ya Afya 2017 katika Mashirika 300 yalichangia zaidi ya ajira 5517 Sekta ya Asasi za Kiraia na inadhihirisha kwamba hiyo ni tanuri la kuandaa Viongozi wa Kitaifa kuanzia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa,
Aliwataja wengine kuwa ni Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Prof Palamagamba Kabudi; Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe Ummy Mwalimu; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji Mhe Prof Kitila Mkumbo; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Suleiman Jafo; Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Ole Nasha; Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Watu wenye Ulemavu Mhe Ummy Nderiananga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Prof Adelardu Kilangi.
Mbunge Neema alielezea kwamba Sekta hiyo ina mchango mkubwa hivyo ushirikiano wao na Serikali utaweza kuleta tija kubwa na kuweza kuwa chachu ya Maendeleo ya Taifa ambayo ni muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi wake na wananchi.
Mbunge Neema alisema hivi sasa Sekta ya Asasi za Kiraia wanakusudia kuandaa Mpango Kazi ambao watauwasilisha kwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa kabla ya kwenda kumuona Mhe Rais kama ambavyo alishaomba.
Kwa kumalizia, Mhe Neema Lugangira alimaliza kwa kusema ndani ya Bunge wapo Wabunge wengi waliopitia Sekta ya Asasi za Kiraia hivyo anaona ipo haja ya kuanzisha Kikundi cha Wabunge wa Vinara wa Azaki yaani NGOs, CSOs na CBOs ili kuimarisha Utekelezaji wa Muongozo wa Uhusishwaji Asasi za Kiraia kwenye Kamati za Bunge ambao umeandaliwa na Bunge.
Hata hivyo alisema kwamba Asasi za Kiraia inapenda kuipongeza Serikali kwa wito wa utashi wa kushirikiana na Sekta Binafsi ili kukuza Ustawi wa Maendeleo ya Jamii na Uchumi wa Taifa.
“Nitumie fursa hii kuikimbusha Serikali kwamba kuna Sekta nyengine ambayo nayo inaweza kuchangia kwenye maeneo ya Taifa ambayo ni Sekta ya Asasi za Kiraia (NGOs, CSOs) kwa sababu sekta hiyo inasifa zote za kuwa chachu ya kuinua na kukweza Dira ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa” Alisema
Alisema hata kwenye Ilani ya CCM imetambua mchango mkubwa wa Asasi za Kiraia kwamba ni muhimu katika kutekeleza mipango ya maendeleo na alifanya rejea ukurasa ya 24 na 128 lakini vivyo hivyo alisema kwamba CCM ndio Chama pekee ambacho kimetenga kwenye nafasi zake za Ubunge Viti Maalumu kuwa Mwakilishi wa Kundi la Asasi za Kiraia ambapo yeye anawakilisha Tanzania Bara na Mhe Khadija Abood anawakilisha Zanzibar.
“Lakini pia napenda kuipongeza Serikali kupitia Msajili wa NGOs kwa kazi kubwa inayofanya kusimamia Utekelezaji wa Sheria za NGOs 2019 na kwa mara ya kwanza imeweza kuchakata na kubainisha ni kiasi cha fedha kinachoingia nchini kwenye sekta hiyo” Alisema
Mbunge Neema alisema kwa kipindi cha miezi sita tu kati ya Julai 2020 Machi 2021 Jumla ya mikataba 178 ilichakatwa na ilifanyiwa upembuzi na ofisi ya Msajili wa NGOS iliweza kubaini jumla ya TZS 546,758,508,322.27 yaani Bilioni 546 Milioni 758, Laki 508 ziliingia nchini kupitia NGOs hivyo Sekta hiyo ina mchango mkubwa sana katika kuendeleza Taifa.
Mbunge Neema aliomba pia itengwe Bajeti ya kutosha kwa Ofisi ya Msajili wa NGOs na Baraza la Taifa la NGOs ili waweze kuendelea kusimamia utekelezaji na utaratibu kwenye sekta hiyo muhimu kwa Maendeleo ya Nchi
Post a Comment