Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA ATEUA MKUU WA ITIFAKI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI NA KUTEUA PIA MKURUGENZI WA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO, LEO


Rais Samia Suluhu Hassan

Ikulu, Chamwino.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amemteua Yusuf Tindi Mndolwa kuwa Balozi na pia kuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Pia Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Miundombinu na Operesheni wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Benedict Benny Ndomba kuwa Mkurugenzi wa  Mamlaka hiyo (eGA).


Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dodoma usiku huu, imesema, Balozi Mteule Mndolwa anachukua nafasi iliyoachwa na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Augustine Ibuge ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


"Balozi Mteule Mndolwa ataapishwa Jumatatu  Aprili 19, 2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma", imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa Ndomba ambaye uteuzi wake umeanza  leo Aprili 17, 2021, anachukua nafasi ya nafasi ya Dk. Jabir Bakari Kuwe ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 17 Aprili, 2021.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana