MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma kupitia tiketi ya CCM, Jacqueline Msongozi amepaza sauti bungeni akilalamikia kitendo cha wabunge wa viti maalumu kunyanyaswa kijinsia, kunyanyapaliwa na kufanyiwa ukatili na vitisho juu na wabunge wa majimbo wanapowajibika kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.
Msongozi aliyasema hayo alipokuwa akichangia bungeni mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo ameiomba serikali kufanya suluhu ya jambo hilo na kwamba wanapanga kwenda kumuona Rais Samia Suluhu Hassan mara atakapopitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM kuwa Mwenyekiti ili awasaidie wawe wanafanya kazi zao kwa uhuru.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video, Mbunge Msongozi akielezea masahibu hayo....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Post a Comment