Na Said Khamis, Kibaha
Serikali imesema itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji nchini katika jitihada zao za uwekezaji kwa kuhakikisha kuwa changamoto watakazozipata zilizopo ndani ya uwezo wake inazisimamia na kuzitatua ili wawekezaji hao waendelee kufanya vizuri kwa ajili ya manufaa yao na nchi.
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipotembelea Kiwanda cha Kuunganisha magari cha GF-Vehicle Assembling, kilichopo Kibaha katika mko wa Pwani kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kiwanda hicho.
Waziri mkuu awataka wawekezaji kuwaalika marafiki zao nje ya mipaka ya Tanzania kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa kuna miundombinu raifiki katika sekta ya uwekezaji.
Pia ametumia fursa hiyo kuupongeza mkoa wa Pwani kwa kuweza kutenga maeneo mengi ya ardhi katika Halmashauri zake zote kuvutia wawekezaji wengi hivyo kuitumia vizuri fursa ya maendeleo ya viwanda nchini.
Awali Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ameeleza kuwa mkoa huo ni wa Viwanda ambapo hadi sasa una vipatavyo 1438 kati yake vikubwa kama hicho cha magari alichotembelea ni zaidi ya 82.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Ali Jawad Karmali amesema GF-Vehicle Assembling Wanajivunia kuwekeza nchini Tanzania na kuwa kiwanda cha kwanza kutengeneza magari nchini.
Karmali ameiomba serikali kuzielekeza Tasisisi zake ikiwemo Majeshi zisiwe zinaagiza magari kamili badala yake ziwe zinaagiza vipuri na baada ya kuviingiza nchini ziwe zinaipa GF-Vehicle Assembling, kazi ya kuunganisha vipuri hivyo na kuwa gari kamili lenye ubora kamili.
Vile vile alisisitiza kuwa anaamini changamoto ndogo ndogo wanazokutana nazo zitatatuliwa kwa kushirikiana na serikali ili kampuni hiyo iweze kushiriki kikamilifu kutimiza kaulimbiu ya Tanzania ya Viwanda.
Kermali amesema hadi sasa Kampuni hiyo ya GF- Vehicle Assembling, imetoa ajira zaidi ya 100 kwa Watanzania ambao wengi wao ni vijana na kwamba ajira hizo zimegawanyika katika sehemu tatu za kugumu, zamikataba na za muda mfupi.
*******
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa akisiliza maelekezo kutoka kwa Baraka Samson, wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Magari GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoani Pwani ldo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Ally Jawad Karmali. Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa akisiliza maelekezo kutoka kwa, Elizabert Mwaya wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha kutengeneza Magari GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoani Pwani leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Ally Jawad Karmali. Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza magari cha GFA-Vehicle Assembling kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani, wakati wa ziara ya kukagua kiwanda hicho leo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo. (Picha zote na Said Khamis)
Post a Comment