Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Baraza la Eid lilofanyanyika katika Stendi mpya ya Kigoma. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
…………………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka wakazi wa Kigoma kufanya kazi kwa uadilifu kwa mustakabali maendeleo ya Taifa, ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kigoma kufuatilia maombi ya ardhi kufanikisha shughuli ya kilimo cha zao la Mchikichi.
Akizungumza katika Baraza la Eid lilofanyanyika katika Stendi mpya ya Kigoma Dkt. Mpango amewata wana Kigoma kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kutekeleza miradi Mikubwa ya kimkakati.
“Tukaendeleze amani, upendo, mshikamano kwa yale tuliyoyafanya ndani ya kipindi cha siku 30 za mfungo, tuendelee kuliombea Taifa letu ili yote tuliyopanga kutekeleza yaweze kukamilika kwa wakati,” alisisitiza Dkt. Mpango.
Aidha, akiendelea na hotuba yake Makamu wa Rais aliongeza kwa kusema kuwa maendeleo katika Nchi yetu yako dhahiri katika sekta ya Afya, Elimu, Maji na Miundombinu ya Reli na Barabara.
Kwa upande mwingine Dkt. Mpango alitumia nafasi hiyo kuwaasa Watanzania kupendana bila kujali tofauti za dini zao.
Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Kigoma katika kutekeleza huduma za kijamii lina miliki Shule tatu za Sekondari na wamemuomba Mgeni rasmi kupatiwa ardhi kwa ajili ya kutekeleza kilimo cha Michikichi pia kujenga Zahanati itakayogharimu takriban Shilingi Bilioni 1.6
Post a Comment