Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi Amandus Chinguile amekabidhi mifuko ya saruji 1,800
Mei 22 /2021 ikiwa ni Moja ya ahadi yake katika sekta ya ELIMU aliyoitoa wakati akiomba ridhaa katika uchaguzi Mkuu 2020.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika kata 16 kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule za sekondari ndani ya kata hizo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Amandus Chinguile alisema 'yeye kama Mbunge anao wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki kwa kuwaboreshea miundombinu.
Alisema kuwa ataendelea kuziangazia shule zenye changamoto na kuziwekea mazingira rafiki ya kujifunzia.
Vifaa hivyo vinatarajia kutumika kakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 22 katika Shule za Sekondari zilizopo Jimboni humo.
"Ni wajibu wetu sisi kama viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja kuinua Elimu katika wilaya yetu kwa kuhakikisha tunaiboresha Miundombinu ya shule"Alisema Chinguile.
Aliongeza kuwa, hii awamu ya kwanza ameziangazia kata 16 katika sekta ya Elimu,akini ataendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika kata nyingine.
'Ili Jimbo liendelee kupiga hatua kimaendeleo nitaendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi kwa kuimarisha miradi ya Maendeleo katika sekta ya Maji,Afya ikiwemo kuisimamia Serikali katika sekta ya Kulimo ili pembejeo za Kilimo ziweze kuwafikia kwa wakati na zipatikane kwa bei nafuu.
Post a Comment