Featured

    Featured Posts

PICHA MBALIMBALI RAIS SAMIA ALIPOONDOKA JIJINI DODOMA NA KUWASILI NCHINI KENYA, LEO

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishuka kwenye Ndege ya Tanzania baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya, akiwa nchini humo atakutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, pia atahutubia Mabunge mawili ya Kenya na kuhutubia Mkutano wa Wafanyabiashara.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wenyeji baada ya kushuka kwenye Ndege ya Tanzania alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisindikizwa baada ya kupokewa aliposhuka kwenye Ndege ya Tanzania baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya.

Wakati akiondoka Nchini kutoka jijini Dodoma kwenda Kenya👇
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na baadhi ya viongozi wakati akienda kupanda Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na Makamu wa Rais Dk. Isdori Philip Mpango wakati akienda kupanda Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza mawili au matatu ya kuagana na Makamu wa Rais Dk. Isdori Philip Mpango, akiwa eneo la mapumziko mafupi wakati akisubiri kwenda kupanda Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipanda Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika mlango wa Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kabla ya kuingia ndani, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.
"Mbakie Salama Wananchi wangu", ni kama ndivyo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alivyokuwa akisema wakati akiaga akiwa kwenye mlango wa Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, mda mfupi kabla ya kuingia ndani tayari kwa safari ya kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo. 
Imetayarishwa na Bashir Nkoromo - CCM Blog
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana