Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka leo Alhamisi Mei 13, 2021 atafanya mkutano na Waandishi wa habari mjini Kigoma.
Taarifa ya Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, imesema Shaka atafanya mkutano huo saa kuanzia nne (4.00), asubuhi katika Ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma, Kigoma mjini.
Katika mkutano huo, Shaka anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa, ikiwemo tathmini ya Kampeni za CCM katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Majimbo ya Muhambwe na Buhigwe mkoani Kigoma.
Shaka anafanya mkutano huo ikiwa leo ni siku ya 10 tangu Kampeni za CCM kuzinduliwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa katika Jimbo la Muhambwe Mei 04, 2021 na siku ya 9 tangu Majaliwa alipozindua Kampeni katika Jimbo la Buhigwe, Mei 05, 2021.
Katika jimbo la Muhambwe bendera ya CCM inapeperushwa na Mgombea wake Dk. Florence Samizi, huku jimbo la Buhigwe mgombea wa CCM akiwa ni Mwalimu Eliadory Kavejulu.
Uchaguzi mdogo katika majinbo hayo unatarajiwa kufanyika Mei 16, 2021, ikiwa kwa Muhambwe inazibwa nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Makamu wa Rais Dk. Isdor Mapngo na la Buhigws kuachwa waziri na aliyekuwa Mbubge wa Jimbo hili Injia Atashasta Nditiye kwa kufariki Dunia.
Post a Comment