Sura za bashasha, ndenremo na vifijo vilitawala wakati Rais Samia Suluhu Hassan akitangazwa mshindi wa Uenyekiti wa CCM wakati wa Mkutaano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ukumbi wa CCM wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Aprili 30, 2021. Mama Samia amekuwa Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo. Amechukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli kufariki Dunia Machi 17, 2021.
Mama Salma Kikwete (katikati)Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne akiungana na wajube wenzie wa Mkoa wa Lini kushangilia ushindi wa Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (wa tatu kulia) akiwa na wajumbe wenzie kutoka Mkoa wa Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika (aliyevaa miwani) akiwa na wajumbe wenzie wa Mkoa wa Njombe wakionesha nyuso za bashasha wakati matokeo ya ushindi wa Rais Samia yakitangazwa kuwa mchindi wa Uenyekiti wa CCM Taifa.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata (katikati) akiwa na wajumbe wenzie Rais Samia akitangazwa kuwa ameshinda kwa kishindo uenyekiti.
Mjumbe wa Mkutan Mkuu Maalumu, amabye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Swale akiwa na furaha kusikia Rais Samia ameshinda kwa asilimia 100 uenyekiti.
Wajumbe kutoka Mkoa wa Mbeya
Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo (aliyevaa shati la kijani), akiwa na wajumbe wenzie wa Mkutano Mkuu Maalumu wakati matokeo ya uchaguzi yakitangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa Rais Samia ameshinda kwa kishindo uchaguzi huo wa mwenyekiti wa CCM.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM amabye ni Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (kulia) akiwa na wajumbe wenzie kutoka Mkoa wa Ruvuma.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Wajumbe kutoka Mkoa wa Iringa
Wajumbe kutoka Mkoa wa Mbeya
Wajumbe kutoka Mkoa wa Njombe. katikati mbele ni Katibu wa Uenezi wa mkoa huo, Erasto Ngole maarufu kwa jina la Shikamoo Parachichi.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini ambaye ni mjumbe wa mkutano huo, Richard Kasesera akishangilia ushindi mkubwa wa Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Sita.
Wajumbe wakitoka ukumbini baada ya mkutano huo kumalizika. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment