Featured

    Featured Posts

WAFUNGWA NA MAHABUSU GEREZA LA MAHABUSU MPANDA WALILIA JAJI

 

Waomba Makatibu Wakuu kutumia vikao vyao na Mhe. Rais kuwaombea Jaji

Waomba matukio ya watuhumiwa kuachiwa na kukamatwa tena yatupiwe jicho

Walalamikia  ubambikiziwaji  kesi

Na Mwandishi Maalum, KATAVI-MPANDA

29/5/2021

Wafungwa na  Mahabusu wa Gereza  Mahabusu Mpanda Mkoani Katavi, wamelalamikia kitendo cha mtuhumiwa  kukamatwa  tena mara tu anapoachiwa na  mahakama na kufunguliwa upya mashtaka na upelezi kuanza tena

Wamesema matukio hayo ni ubinyaji wa mnyororo mzima wa utoaji Hakijinai  kwa wakati.

Wafungwa na Mahabusu hao wameyasema hayo   mwishoni mwa mbele ya Makatibu Wakuu, Sifuni Mchome , Laurian Ndumbalo na John Jingu ambao  kwa pamoja  walitembelea Gereza  Mahabusu  Mpanda  na kuzungumza na Maafisa, Askari pamoja na Wafungwa na Mahabasu kwa lengo la kujifunza   mafanikio na changamoto  katika chombo hicho cha utoaji wa Hakijinai.

“ Waheshimiwa  Makatibu Wakuu, sisi wafungwa  na mahabusu wa Gereza Mahabusu Mpanda, tunatumia nafasi hi kuwaeleza kuwa tatizo la upatikanaji  haki kwa wakati limekuwa sugu katika Mkoa wetu wa Katavi. Na jambo la kusikitisha ni kwamba, mtuhumiwa anakaa Gerezani zaidi ya miaka  mitatu hadi mine, anapofikishwa mahakamani kesi hiyo inafutwa, lakini hapo hapo mtuhumiwa anakamtwa tena na kesi inaanza  upya kana kwamba ndiyo kwanza amekamtwa” akasema  msoma risala  Paulo Ulaya na kushangiliwa na   wafungwa na mahabusu wenzie.

Katika risala yao kwa Makatibu wakuu hao na mbele ya   Mkuu wa Magerea  Mkoa wa Katavi ACP Wilson Rugamba na  Mkuu wa Gereza  hilo, SP Moses Mbesela na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzuga, wafungwa na mahabusu hao, wakasema

 “ Huu ni uonevu   kwa kuwa  mtuhumiwa anakuwa amekaa miaka mingi  na kuteseka gerezani. Tena cha kusikitisha hata upelelezi unaanza upya na kuchukua muda mrefu sana wakati  upelelezi wa kwanza ulishakamilika”

Wafungwa  na mahabusu hao walitoa mifano ya  kesi  nne  ambazo zilifutwa na  watuhumiwa kukamatwa tena, na hivyo wakawaomba Viongozi hao wasaidie katika eneo hili. Na kukomeza   uonevu huo unaofanywa na Jeshi la  Polisi kuwatesa wananchi wananchi. 

Kuhusu  ucheleweshaji wa  usikilizwaji wa mashauri yao, wafungwa na mahabusu wa Gereza hilo, wameelezea shauku yao ya kuta awepo Jaji wa Mkoa wa Katavi.

“Sisi wafungwa na mahabusu tunayoheshima kubwa kuwaeleza shauku yetu kuwa tuna tamani na sisi kuletewa Jaji katika Mkoa wetu wa Katavi yaani kuwepo kwa Mahakama Kuu  Katavi kutokana na kwamba idadi kubwa ya mahabusu katika gereza hili ni kesi za mauaji ambazo hatima yake inamuhitaji Jaji” wakatoa rai wafungwa hao

Vile vile wamesikitikia kitendo cha kesi za muda mrefu kutopewa kipaumbele katika vikao na wakatoa mfano wa kesi  nne ambazo ni za muda mrefu na bado hazijapewa kipaumbele cha kusikilizwa.  Na  wakaomba  wasaidiwe   kulisemea jambo hili katika vikao na Mhe. Rais ili basi na  wao wa Mkoa wa Katavi  wapatiwe  Jaji ili  pia isaidie kupunguza msongamano .

Kwa sasa kesi zote za mauaji   zinasikilizwa Mkaoni  Rukwa ambapo inabidi mahabusu wasafirishwe kutoka Mkoani  Katavi jambo ambalo kwa Mujibu wa Mkuu wa Gereza hilo SP Moses Mbesela   si salama lakini wakati mwingine mahabusu wanashindwa kupelekwa  Rukwa kwa ukosefu wa Usafiri  ambao ungeweza kuwachukua  mahabusu wengi kwa wakati mmoja.

Robo tatu ya mahabusu katika Gereza hilo wanakabiliwa  na  kesi za mauaji,

Aidha Wafungwa na mahabusu hao wameitaja changamoto nyingine inayobinya myororo wa utoaji haki katika Mkoa wa Katavi ni pamoja na tatizo la  kumbakikiziwa kesi.

“Tunaomba tutumie pia nafasi hii kuwaeleleza  kuwa katika Mkoa wetu  tumekuwa na tatizo la polisi kuwabambikizia kesi wananchi wenu, hivyo tunaomba  Mhe. Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria uunde tume yako ichunguze kwa undani kuhusu suala hili na ndio maana utagundua kesi nyingi upepelezi wake haukamiliki kwa wakati kutokana na mazingira ya uundaji wa kesi hewa” wakalalamika wafungwa na mahabusu hao.

Vile vile  mahabusu na wafungwa hao wamelalamikia kitendo cha Mahabusu kutoka Mahakama ya  wilaya ya Mlele kutopelekwa mahakamani kwa wakati na kwamba wanaomba wasaidie  kutokomeza uonvu huo ili na wao wapate kujua hatima ya kesi zao.

Aidha wafungwa na mahabusu hao wameomba Makatibu Wakuu hao  kuwasaidia kutokomeza uonevu wa  unaofanywa na Polisi wa kushikilia mali za watuhumiwa kwa madai ya kuwa ni vielelezo.

Walitaja pia mifano ya kesi nne ambazo watuhumiwa mali zao zinashikiliwa na polisi, mali ambazo wanasema nyingine zingeweza kusaidia  familia zao wakati wao wakiendelea kusubiri hatima yao. 

Gereza Mahabusu Mpanda lilianzishwa mwaka 1947, likiwa na uwezo wa  kuhifadhi wahalifu 100. Lakini  kwa sasa lina jumla ya wahalifu 333 na wakati mwingine  wanafika hadi 400.

Pamoja na idadi hiyo kubwa ya   mahabusu na wafungwa, Gereza Mkoa wa Katavi lina watumishi 59 ambapo Maafisa ni wanne, na askari wa cheo cha Rank and file ni 55 na hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 21 kwa mchanganuo wa Maafisa 6 na askari wa kawaida 15 kwaajiili  kukabiliana na  shughuli ya ulinzi wa wafungwa na  mahabusu.

Makatibu Wakuu  Profesa Sifuni Mchome ( Katiba na Sheria), Dkt Laurian Ndumbalo (Utumishi) na Dkt, John Jingu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  wakijadiliana jambo na viongozi wa Magereza  Mkoa wa Katavi mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo yao na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Mpanda 
ambako wafungwa na mahabusu  pamoja na mambo mengine  wameomba Mkoa huo upatiwe Jaji
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana