Featured

    Featured Posts

BALOZI NJOOLAY AAGWA, APONGEZWA, AIMWAGIA SIFA MKURABITA KWA UCHAPAKAZI


Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Baiashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita anayemaliza muda wake, Balozi mstaafu Daniel Njoolay (alivaa fulana ya mistari) wakiwaongoza wajumbe wa Bodi, menejimenti na  watumishi mpango huo kucheza muziki wakati wa hafla ya kuagwa kwa Bodi ya wakurugenzi iliyomaliza muda wake wa miaka mitatu, juzi jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, anayemaliza muda wake, Balozi mstaafu Njoolay akicheza muziki na mmoja wa watumishi wa Mkurabita.
Balozi mstaafu Njoolay akifurahia jambo pamoja na Dkt Mgembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkurabita, Dkt. Mgembe akizungumza wakati wa hafla hiyo , kwa kuipongeza Bodi ya Wakurugenzi kwa kazi nzuri na yenye mafanikio waliyoifanya wakati wa kipindi chao cha miaka mitatu ndani ya Mkurabita..
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkurabita, Mujungu Masyenene akiishukuru Bodi ya Wakurugenzi inayomaliza muda wake kwa ushirikiano mkubwa walioufanya wakati wa uongozi wao.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Mkurabita, Glory  Mbilimonya akiongoza hafla hiyo.

Sasa ni wakati wa kurebuka







 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkurabita anayemaliza muda wake, Balozi mstaafu, Njoolay (aliyekaa katikati) akiwa na wajumbe wa bodi pamoja na baadhi ya watumishi wa Mkurabita.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 

Na Richard Mwaikenda, Dodoma

 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), anayemaliza muda wake, Balozi mstaafu Daniel Njoolay ameishukuru Menejimenti na watumishi wa mpango huo kwa kuwa wasikivu kutekeleza maagizo waliyokuwa wanawapatia ndani ya miaka mitatu ya uongozi wao.

Balozi Njaalay, ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya Mkurabita kuiaga bodi hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa Mkurabita katika Hoteli ya Corina, jijini Dodoma.

Njoolay amesema kuwa usikivu na uchapakazi wao ndiyo umesababisha Mkurabita kuwa na mafanikio makubwa na kuwataka waendelee na moyo huo na kuisapoti Bodi nyingine itakayokuja baada ya wao kuondoka.

"Kwa niaba ya wajumbe wenzangu napenda nichukue nafasi hii kuishukuru menejimenti, mmekuwa wasikivu kwa yale maelekezo tuliyokuwa tunawapatia asanteni sana. Pili niwashukuru wajumbe wenzangu wa bodi sijapata shida kama kiongozi walinipa ushirikiano mzuri, tunaongea vizuri, hakuna kufokeana tunaelewana na kufikia makubaliano." amesema Njoolay.

Aidha ili kuboresha utendaji na mahusiano kazini, Balozi Njooalay ameutaka uongozi wa Mkurabita kuanzisha Family Day itakayowajumuisha viongozi, watumishi na familia zao ambapo watacheza kwa pamoja na kufahamiana zaidi.

Amesema kuwa wakifanya hivyo utendaji kazini utaongezeka bila wao kujua, lakini pia mchanganyiko huo utaongeza uhusiano miongoni mwao na kuwa wamoja.

Ametoa mfano kuwa akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, alianzisha Family Day baada ya kuwakuta wafanyakazi hali yao ikiwa si nzuri, kitendo ambacho kiliamsha ari ya ufanyakazi na kujenga uhusiano mzuri miongoni mwao na familia zao kwa ujumla.

Pia, akiwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, baada ya kukuta hali ya utengano kati ya watumishi wa kawaida na maofisa wa ubalozi, aliamua kuanzisha Family Day, jambo ambalo lilisaidia sana kujenga umoja na utendaji kazi ukaongezeka. Alipowatangazia kuwa anarejea nchini watumishi ambao asilimia kubwa walikuwa ni wanigeria walilia machozi na kusababisha hata yeye kulia.

"Mchango wenu kwa muda wa miaka mitatu mliokuwa nasi ni mkubwa sana, si kwa kusifia tu, bali huo ndiyo ukweli, kuna vitu mmefanya vinavyotufanya sisi tufuate, Uongozi  wa kutufanya  tukusikilize, tusikie hamu ya kutekeleza  uliyoyasema na bodi yako, tunawashukuru sana," ameanza kwa kusema hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mkurabita, Dkt Seraphia Mgembe.

Dkt. Mgembe amesema kuwa moja ya mambo aliyomuachia Njoolay atakayokumbuka daima na kuendelea nayo katika uongozi wake ni kwamba ukiwa kiongozi kabla ya kumfanyia jambo mtu mwingine au mfanyakazi wako "Lionje kwanza  ukikuta chungu usimfanyie mfanyakazi, na ukionja ukikuta tamu basi mfanyie. kwa kipindi chote  cha ufanyakazi wako Njoolay  umekuwa ukifanya hivyo," amesema Dkt Mgembe.

"Kwa kipindi cha uongozi wenu utekelezaji wa maelekezo yenu umeleta chanya Mkurabita, tunawashukuru sana kwa uongozi wenu mwema, tunaamini huko mwendako mtakuwa mabalozi  muisemee vizuri Mkurabita ili urasimishaji usonge mbele," hayo ni maneno ya
Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi na Biashara wa Mkurabita, Jane Lyimo.

 
Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkurabita,
Mujungu Masyenene amesema kuwa uwepo wa bodi hiyo yenye watalaamu wengi, wamejifunza mengi na kuwafanya iwe rahisi kutekeleza malengo yao, na kwamba wataendelea kufanya mawasiliano nao ili waendelee kuchota utalaamu huo kwa lengo la kuendelea kuboresha ajenda ya urasimishaji nchini.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana