Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mkuu wa Wilaya ya Ubunge Kisare Makori kupitia Uenyekiti wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya hiyo, ameingilia kati ili kuepusha kutoweka kwa usalama katika mgogoro wa eneo la ekari 16 lililopo Goba Kisauke, uliopo baina ya familia mbili tofauti.
Famili zinazohusika katika mgogoro huo ni ya Romane Mazewa Mosha na ya Tabia Mziwanda ambaye imeelezwa kwamba kwa sasa ameshafariki dunia.
Katika kuingilia mgogoro huo ili kufanya usalama utamalaki, juzi DC Makoria alifa ya kikao cha wazi kati yake na familia zinazohusika, ambacho kilifanyika karibu na eneo la le ye mgogoro na kuhudhuriwa na viogozi wa Kata ya Goba na wa Halamashauri ya Manispaa ya Ubungo akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatice Dominic.
DC Makori, katika kikao hicho ambacho kilitanguliiwa na Afisa Mipango miji wa Manispaa ya Ubungo kutoa taarifa nzima ya mwenendo wa mgogoro huo, alikihitimisha kwa kuiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, kuendelea kusimamia usalama na kuhakikisha kuwa eneo hilo halivamiwi au kutumiwa na yeyote mpaka pale mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi.
"Sasa, kwa hatua hii, naiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia kwa Mkurugenzi wa Manispaa, kuendelea kusimamia usalama na kuhakikisha kuwa eneo hilo halivamiwi au kutumiwa na watu ambao hawana uhalali wa kulitumia mpaka pale mgogoro ulioletwa Serikalini ambao bado unashughulikiwa kwa sasa na ngazi ya juu ya Wilaya utakapotolewa maamuzi yake ya mwisho kuhusu mmiliki halali wa eneo hili.
Pili, natoa maelekezo kwa niamba ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa familia ya Mziwanda kuacha tabia ya kuendeleza uvamizi wa kuleta watu katika eneo hili na kuwauzia, badala yake wasubiri malalamiko Setikalini yapate ufumbuzi kama walivyoomba, na jambo hili linashughulikiwa kama tulivyosomewa taarifa hapa na Afisa mipangomiji.
Endapo maelekzo haya yatakiukwa na kuna mtu ataendelea kufanya miamala ya kuwauzia watu kufanya maendeleo katika eneo hili tutachukua hatua za kisheria.
Pia naelewa kuwa kuna eneo ambalo ndani ya eneo hili la mgogoro Roman Mosha anazo hati za kumiliki, pale amejenga nyumba, mara ya mwisho kufika hapa lilikuwa halijaisha kujengwa na nilielekeza yasifanyike maendeleo wakati mgogoro bado unashughulikiwa serikalini, taarifa nilizonazo jengo lile limeshakamilika na kuna mtu anaishi, naagiza jengo lile lifingwe", akasema DC Makori.
DC Makori aliwaomba pia Waandishi wa habari kuwa makini katika kuandika habari kuhusu mgogoro huo, ambapo alisema kumekuwa na chombo kimoja ambaacho hakukitaja, kuwa kimekuwa kikiandika habari za upande mmoja tu unaohusika huku kikiwa hakitafuti pande nyingine zinazokuwa zinaguswa katika taarifa kwa namna moja au ngingine.
Amesema chombo hicho (siyo CCM Blog au Uhuru), kimekuwa kikimtaja Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo katika uandishi ambao unaonyesha kuwa Mkurugenzi amekuwa akishughulikia mgogoro huo wa eneo kama yeye binasi na siyo kama Mkurugenzi wa Manispaa jambo ambalo DC Makori alisema siyo sahihi.
"Hili la nne, ni rai kwa Waandishi wa habari. Niwaombe sana, Waandishi wa Habari ni Wadau wakubwa sana wa ulinzi wa amani na maendeleo katika nchi, Kalam za waandishi zinaweza zikasaidia nchi kuivuka kwenda kwenye maendeleo, lakini pia zinaweza zikatumbukiza nchi shimoni", alisema DC Makori huku akitoa mfano wa nchi jirani (hakuitaja) ambayo alisema ilitumbukia kakati machafuko kwa sababu tu ya kalamu ya mwandishi wa habari.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwenendo wa mgogoro huo iliyotolewa kikaoni hapo na Afisa Mipangomiji, eneo lenye mgogoro ni Shamba namba 2906, 2807, 2808, 2809 na 2810.
Inaelezwa kwamba mbali na familia za Mosha na Mziwanda kugombea eneo hilo, Halmashauri ta Manispaa ya Ubungo nayo inahusishwa katika mgogoro huo kwa kulalamikiwa kuwa inapora eneo la familia ya Mziwanda.
Afisa Mipango miji anaeleza kwenye taarifa yake kwamba chanzo cha mgogoro huo kimetokana na familia ya Mosha kumilikishwa enee hilo ambalo awali lilijulikana kama eneo la Shamba la Kijiji na kupewa nyaraka za Umiliiki, huku familia ya Mziwanda ikiamini kuwa ni eneo la familia ambalo wamerithi kutoka kwa marehemu Said Said Mziwanda na Mosha anamiliki kipande cha ekari 4 tu.
"Eneo linalobaki la takriban ekari 16, ingawafa.ilia ya Tabia Nziwanda wanatambua kuwa eneo lao ni ekari 10 kuwa ndiyo eneo ambalo walilirith kutoka kwa baba mzazi wa Bi Tabia ambaye alikuwa akkijulikana kama Said Said Mziwanda ambaye alikuwa Diwani wa Goba enzi hizo", anasema Afisa mipango miji wa Manispaa ya Ubungo.
Anasema, mwaka 1993 Kamati ya Kijiji cha Goba iliuza eneo la ekari 4 kwa Roman Mazewa Mosha kwa sh. 100,000 na kwamba Kamati iliyouza kipande hicho ilikuwa na wajumbe watano ambao ni Awazi Waziri, Said Duma, Said Pembe, Pazi Kondo na Said Said Said Mzuwanda ambaye ni Baba yake Tabia Mziwanda na ndiye alikuwa Diwani wa Kata ya Goba wakati huo.
"Aidha, kuna mikataba mingine miwili inaonyesha ndugu Roman Mosha kuuziwa eneo na viongozi wa kijiji ambao ni walewale waliokuwepo kwenye Kamati ya Kijiji wakati ikiuza ekari 4, katika mikataba hii miwili hakuna sehemu ambayo inaonyesha ndugu Mosha aliuziwa eneo na viongozi wa kijiji la ukubwa kiasi gani", anasema Afisa mipango miji huyo.
Afisa mipangomiji huyo, aliendelea kusema kwene kikao hicho kuhusu nyaraka za umiliki sa shamba, Ushiriki wa Halmashauri ya Ubungo katika Mgogoro huo, kuainisha madai ya Tabia Mziwanda na Shauri lilivyofika kwa mkuu wa Wilaya ya Ubungo.
Alieleza pia kikao kilichofanyika kati ya Timu kutoka Halmashauri ya Ubungo na Mosha, Kikao na Wanannchi, Timu ya kushughulikia mgogoro huo na Mapendekezo yaliyotolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori akizungumza na kutoa maelekezo kwenye kikao hicho.
Post a Comment