'Mimi naheshimu mawazo ya kila mtu, mtu akinifurahia, akinitukana akinisema mimi nashukuru', alisema Diamond kupitia kituo cha TV cha Wasafi, anachokimiliki.
Diamond ambaye hajatoa nyimbo kwa zaidi ya miezi sita sasa, tangu jina lake litajwe mwezi Mei mwaka huu kuwania tuzo hizo za BET kumeanzishwa harakati za kumpinga msanii huyo mitandaoni ili aondolewe au asishinde tuzo hizo za mwaka huu za BET.
Ni tuzo kubwa duniani, zinazohusisha wasaniii weusi duniani wenye asili ya Afrika.
Wanaompinga msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii wanadaiwa kufanya hivyo ili kuonesha hisia zao kutokana na msanii huyo 'kushiriki siasa akikiunga mkono chama tawala cha CCM' nchini humo, kilichoshinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unaolalamikiwa kuwa na ulikuwa wa udanganyifu licha ya Tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania kusema ulikuwa huru na wa haki.
Lakini pia wanadai kwamba msanii huyo yuko karibu na wanasiasa, wanaodaiwa kukiuka haki za binadamu.
Diamond anayetamba na wimbo 'Waa!' aliomshirikisha gwiji la muziki kutoka DRC, Koffi Olomide, licha ya kuhaidi kulizungumzia rasmi suala hili la kupingwa kwake kwenye tuzo hizo siku chache zijazo, alisema hatachukia mtu anayemsema vibaya.
'Epuka sana kumchukia mtu anayezungumza kitu kibaya juu yako, huwezi kujua, kaamka leo kavurugwa hasira zake kakumalizia wewe, kesho mwenyewe akikaa atajuta na kukuomba msamaha', alisema.
Post a Comment