Featured

    Featured Posts

MAMBO YA BUNGENI DODOMA LEO, NI BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dkt.Festo Dugange akizungumza na na watendaji kata kutoka jimbo la Msalala wliotembelea Bunge Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya wizara hiyo ili ijadiliwe na wabunge bungeni Dodoma .
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi akijibu maswali ya wabunge bungeni Dodoma.
Baadhi ya wabunge kutoka Mkoa wa Mtwara wakijadliana jambo kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma.
Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Mlimba,   Dodwin Kunambi bungeni Dodoma.
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akichangia mjadala wa Bejeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo aliishauri Serikali kurekebisha baadhi ya sheria zinazodhoofisha utalii ikiwemo uwindaji ambapo hivi sasa inaonekana  idadi ya wawindaji imeshuka hadi 8000 kutoka 1500.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Dkt. John Pallangyo akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Mvumi,Livingstone  Lusinde (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi Rais (Kazi Maalumu),  George Mkuchika bungeni Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene Dodoma leo wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama.
Mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga akichangia mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni Dodoma ambapo aliiomba serikali kukamilisha ujenzi wa soko karibu na Daraja la Magufuli.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiingia bungeni


Naibu Wazitri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gekul
Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga akiwa viwanja vya Bunge tayari kuingia bungeni kushiriki mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo akiwa viwanja vya Bunge tayari kuwahi kuingia bungeni kuhudhuria mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Baadhi ya wageni wakifuatilia mwenendo wa Bunge wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni.

Wageni wa Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson kutoka Mbeya wakitambulishwa bungeni Dodoma.
Mbunge wa Liwale, Zubeiry Kuchauka akichangia majadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kilimanjaro, Shally Raymond akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni Dodoma.

 Mbunge wa Meatu, Leah Komanya akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo aliiomba serikali kuweka kambi maalumu ya askari wanayama pori Meatu wa kuwadhibiti Tembo wanaoshambulia makazi ya watu na kuua. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana