CCM Blog, Dar es Salaam, leo
Mwandishi wa Habari nguli ambaye amewahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani yaliyokuwa yakichapishwa na Uhuru Publications Ltd ambayo sasa yanachapishwa na Uhuru Media Group Ltd, Mkinga Mkinga amefariki dunia.
Taarifa za awali zimesema, Mkinga ambaye amewahi pia kuwa Mhariri katika vyombo vya habari hapa nchini, amefariki leo alfajiri katika Hospitali ys Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi kuhusiana na kifo au msiba huo bado hazijapatikana.
Msimamizi Mkuu wa Blog hii na timu yote, tunatoa pole kwa Ndugu, Jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
Mkinga Mkinga akizungumza kwenye kikao chake na wafanyakazi wa Uhuru na Mzalendo alipokuwa Mhariri Mtendaji wa UPL miaka kadhaa iliyopita.
Post a Comment