Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo nchini Msumbiji baada ya Kikao cha dharura cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jana, Juni 23, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Joaquim Chissano Maputo Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais Dk. Philip Isdor Mpango alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma jana, Juni 23, 2021, akitokea Maputo Nchini Msumbiji alikohudhuria Kikao cha dharura cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.
Post a Comment