Mmm |
Rais Samia, jijini Mwanza leo.
CCM Blog, Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Madini kubuni mbinu sahihi za kudhibiti mianya inayopelekea madini aina ya Tanzanite kutopewa thamani inayostahili.
Amemuomba Waziri wa Madini Mhe.Doto Biteko kukaa na wawekezaji na kuhakikisha madini ya ‘Tanzanite’ yanasaidia kuleta maendeleo.
Ametoa maagizo hayo leo katika ziara yake ya siku tatu Jijini Mwanza ambapo amezindua kiwanda cha kusafisha madini ya dhahabu mkoani huo pamoja kufungua jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kanda ya Ziwa.
Ameitaka Wizara ya Madini kuwasaidia wachimbaji wadogo na wakubwa wa dhahabu ili wachimbe dhahabu ya kutosha kukidhi mahitaji ya kiwanda cha kusafisha dhahabu Jijini Mwanza.
“Mwanza ni dhahabu mkilia umasikini ni uzembe wenu lakini Mungu alishusha utajiri wa kutosha Mwanza lakini na viongozi wenu Mungu aliwatia akili ya kuleta mitambo na mambo mengine yakusafisha utajiri mliopewa na Mungu ili Mwanza ineemeke na ninavyosema hivyo nitumie jukwaa hili kumshukuru kwa dhati ingawa hatuko nye Rais wa Awamu ya tano kwa sababu mageuzi haya tuliyafanya chini ya uongozi wake.”Amesema Rais Samia.
Aidha Rais Samia amesema kupitia mtambo wa kusafisha dhahabu utawezesha Benki kuu ya Tanzania BOT kuanza kununua dhahabu kwa mujibu wa sheria na hivyo kuwezesha nchi kuwa na amana ya dhahabu yaani Tanzania sasa itaanza kuwa na ‘gold reserve’
Post a Comment