Featured

    Featured Posts

SH. BILIONI 34 KUTUMIKA KUSAMBAZA UMEME VIJIJI 114 MKOANI KAGERA KUPITIA REA


 Na Lydia Lugakila, Muleba
Jumla ya Sh. bilioni 34 zinatarajiwa kutumika katika usambazaji umeme kwa  vijiji 114 Mkoani Kagera kupitia Mpango wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili huku sh. bilioni 6 zikitumika kwa wilaya ya Muleba.

Amebainisha hayo naibu waziri wa nishati Stephano Byabato katika uzinduzi rasmi wa mpango huo wa REA uliofanyika katika Kijiji cha Omurunazi kata ya Mushabago  wilayani Muleba Mkoani Kagera ambapo amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitatumika katika kuwaunganishia umeme wananchi wa mkoa huo.

Byabato amesema kuwa shilingi bilioni 6 zitatumika kusambaza umeme katika vijiji 166 ambapo amesema kwa hadi Sasa vijiji 100 tayari vimekwisha pata umeme na vijiji 66 havina huku harakati zikiwa ni kupatiwa umeme katika wilaya hiyo.

Naibu waziri huyo amewahimiza wananchi mkoani humo kutumia fulsa hiyo kujishughulisha katika shughuli za kujiongezea kipato kwa kutumia nishati hiyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo, ujasiliamali huku akisisitiza wananchi kuupokea mradi huo na kuutunza na kuwa hakuna mwananchi atakayeuziwa nguzo kwani ni bure.

Aidha katika shughuli ya uzinduzi wa mradi huo naibu waziri huyo ametoa kiasi cha shilingi laki 2 na elfu 70 kwa ajili ya kuwaunganishia wananchi 10 wa Kijiji cha Omurunazi.

Naye mbunge wa Muleba kaskazini Charles John Mwijage amewaomba wananachi kuendelea kuvuta subira wakati zoezi hilo likiendelea na kuwataka wakandarasi wa shughuli hiyo kumaliza kwa wakati na kwa uaminifu ili kupata miradi mikubwa zaidi.

Hata hivyo kwa upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa wakala wa nishati vijijini REA mhandisi Romanus Lwena amesema kuwa hakuna Kijiji hata kitakachobaki kupatiwa umeme.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana