Ikulu Dodoma, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewateua Suleiman Yusuph Mwenda na Lupakisyo Andrea Kapange kwa Wakuu wa Wilaya mbili tofauti.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, imesema Mwenda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
Kabla ya uteuzi huo, Mwenda alikuwa Katibu Msaidizi Idara ya Oganaizesheni ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu Jijini Dodoma na amechukua nafasi ya Kenan Laban Kihongosi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa UVCCM.
Taarifa hiyo imesema Lupakisyo Andrea Kapange ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kuchukua nafasi ya Dk. Charles Mhina ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Kapange alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Tanga.
Uteuzi wa Wakuu hao wa Wilaya umeanza Juni 22, 2021.

Post a Comment