NA MWANDISHI WETU, WINDHOEK, NAMIBIA.
TANZANIA imeendelea kung'ara ndani ya Bara la Afrika kwa kutangaza vyema vivutio vyake vya Utalii ambapo imeweza kuwa miongoni mwa nchi 10 bora kwa mwaka wa tatu mfululizo, kuanzia 2017 hadi 2020.
Ripoti hiyo imetolewa mapema leo kwenye mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Utalii Duniani (UNWTO), Mtaalamu wa utangazaji wa Utalii, Bi. Olga Nowak aliitangaza Tanzania kushika nafasi ya saba ambayo inakuwa ni mara ya tatu.
Katika kumi bora hiyo, Afrika ya Kusini imetajwa kushika nafasi ya kwanza ikifutiwa na nchi ya Misri katika utangazaji vyema ya vivutio vyake vya utalii.
Aidha katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa kuendelea kuongoza na kufanya vizuri katika sekta ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa UVIKO19 ambao umeikumba karibu Mataifa mbalimbali duniani kote.
Tanzania imekuwa na vivutio mbalimbali vinavyotamba Duniani ikiwemo mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi zenye vivutio vikubwa vya Wanyama kama Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Nyerere, Hifadhi ya Ruaha, Tarangile,l pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro
Katika hatua nyingine Tanzania kushiriki katika mkutano huo kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ndumbaro na wataalamu imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususan viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali kwa kufanya vikao vya ana kwa ana na viongozi wanaoshiriki mkutano huo
Pia, Tanzania imepata fursa ya kutoa maoni yake kwa lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara la Afrika ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amemkaribisha Mtaalamu wa masuala ya utangazaji kuja Tanzania kutoa ujuzi huo.
Post a Comment