Sehemu ya wajumbe wa baraza
Wajumbe wa Baraza wakiwa wamesimama kuonesha mshikamano wakati wa kuhitimishwa kwa kikao cha baraza.
Viongozi wa Tughe Taifa wakipiga makofi wakati wa kuhitimisha kikao hicho cha Baraza.
Mwenyekiti wa Tughe Mkoa wa Pwani, Catherine Katele akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Tughe Taifa, Achie Mntambo (kushoto) na Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Herry Mkunda.
Naibu Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Aman Msuya (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Herry Mkunda.
Wenyeviti wa Tughe wa mikoa wakipiga makofi wakati wa kumkabidhi zawadi ya kitenge, Mwenyekiti wa Tughe mkoa wa Pwani, Catherine Katele ikiwa ni shukrani kwake kwa kuwa kiunganishi kikubwa wa umoja wa wenyeviti hao.
Mwenyekiti wa Tughe Taifa, Mntambo (kulia) akimkabidhi zawadi ya kitenge, Mwenyekiti wa Tughe Mkoa wa Pwani, Catherine Katele iliyotolewa na wenyeviti wenzie wa mikoa kwa kutambua mchango wake mkubwa kuwaunganisha kuwa wamoja.
Catherine akipongezwa na wenyeviti wenzie.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
TAMKO LA BARAZA KUU TUGHE TAIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU KANUNI MPYA ZA MAFAO YA PENSHENI KWA WASTAAFU, LEO TAREHE 11 JUNI 2021 KATIKA UKUMBI WA ST GASPER JIJINI DODOMA
Utangulizi
Ndugu waandishi wa Habari, Leo Tarehe 11Juni2021,Baraza Kuu Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) tumekutana katika Kikao Maalum kufuatia maazimio ya Kikao cha Baraza Kuu la Chama laTarehe 30-31 Desemba 2020 Mjini Morogoro.
Pamoja na mambo mengine katika kikao hiki, wajumbe wamepata fursa ya kufahamishwajuu ya hatua zilizofikiwa katika Utekelezaji wa Maagizo ya Serikali ya Tarehe 28 Desemba 2018ambayo yalihusu kurejewaupya wa Kanuni za Mafao ya Wastaafu za Mwaka 2018 kwa kuwashirikisha wadau wote wa Hifadhi ya Jamii.
Akitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wake na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Ikulu Jijini Dar es Salaam,aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli alielekeza, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini yaani NSSF na PSSSF wasitishe matumizi ya Kanuni Mpya za Mafao za Mwaka 2018 katika ulipaji wa Mafao ya Uzeeni kwa Wastaafu na kuendelea kutumia Kanuni za Awali za kila Mfuko.
Aidha, Serikali iliagiza kuwepo kwa kipindi cha mpito cha miaka mitano (2019 –2023), na kuitaka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu ianzishe Mchakato wa kupitia upya Kanuni hizo kwa kuwashirikisha kikamilifu wadau wote wakiwemo Waajiri na Vyama vya Wafanyakazi ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazimahapo baadaye.
Ndugu waandishi wa Habari, TUGHE tunaridhishwa nahatua zilizofikiwa za utekelezaji wamaagizo ya Serikali.Tunaishukuru na kuipongeza sana Serikali Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza ushirikishaji wa wadau wote wa Hifadhi ya Jamii wakiwemo wawakilishi wa Vyama vya Wafanyakazi kupitia TUCTA.
TUGHE tumejulishwa kuwa Serikali kwa kushirikiana na Wadau imeunda Kamati mbili ambazo ni Kamati Elekezina Kamati ya Wataalamambazo zitapitia kwa undani hali ya mifuko kwa lengo la kuishauri Serikali juu ya Kanuni Bora ya Mafao itakayowanufaisha Wanachama na kulinda uhai wa Mifuko.Aidha,tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Uongozi wa Mifuko yote miwili ya NSSF na PSSSF kwa kuendelea kutekeleza maagizoya Serikali ya kuendelea kulipa mafao kwa Wastaafu kwa kutumia Kanuni za awali kabla ya ujio wa Kanuni za 2018.
TUGHE tunafahamu kuwa, katika kipindi cha mpito cha miaka mitano, Mfuko wa PSSSF unaendelea kuwalipa mafao waliokuwa Wanachama wa Mifuko ya LAPF na PSPF kwa kutumia kilimbikizi cha1/540 (Annual Accrual Factor), Kadirio la muda wa kuishi baada ya kustaafu miaka 15.5(Commutation Factor), kiwango chamalipo ya mkupuo cha50%ya Pensheni ya Mwaka(Commutation Rate)na kiasi kinachobaki cha50% cha Pensheni ya Mwaka kinatumika kulipapensheni ya kila mwezi.
Wanachama wa iliyokuwa mifuko ya GEPF na PPF wao pia wanaendelea kulipwa Mafao yao kwa kutumia kilimbikizi cha1/580(Annual Accrual Factor), Kadirio la muda wa kuishi baadaya kustaafu miaka 12.5(Commutation Factor), kiwango chamalipo ya mkupuo cha25%ya Pensheni ya Mwaka(Commutation Rate)na kiasi kinachobaki cha75% cha Pensheni ya Mwaka kinatumika kulipapensheni ya kila mweziKanuni ambayo pia inatumika kuwalipa Mafao Wastaafu wa Mfuko wa NSSF.
Ndugu waandishi wa habariKupitia Tamko hili, TUGHE tunaendelea kusisitiza na kuikumbusha Serikali pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuwa, ni vyema kabla ya kufikia mwisho wa kipindi cha Mpito na kabla ya kutangazwa kwa Kanuni Mpya, itolewe elimu ya kutosha kwa Wadau wote wa Hifadhi ya Jamii Nchini hasa Wafanyakazi.
TUGHE tunaamini kuwa, iwapo elimu ya kutosha itatolewa kwa Wanachama wa iliyokuwa Mifuko ya LAPF na PSPF juu ya dhamira nzuri ya Serikali ya kufanya maboreshohifadhi ya Jamii kwa kupendekeza matumizi ya Kanuni bora yenye kujali hali za Wanufaika wa Penshenina Uhai wa Mifuko, Watumishi hawa wataelewa na hivyo kuondoa uwezekano wa kuzuka kwa mgogoro mwingine wa kupinga Kanuni pale itakapotangazwa.
MATARAJIO YA WANACHAMA WA TUGHE NA WATUMISHI WOTE WA UMMA KWA UJUMLA
Ndugu Waandishi wa Habari
Kama tulivyoeleza hapo awali, Wanachama wa TUGHE kama walivyo wafanyakazi na Wadau wengine wa Hifadhi ya Jamii hapa Nchini, tunafahamu nia nzuri ya Serikali yetu ya kuhakikisha Wastaafu wa Kada zote wanapata hifadhi ya jamii iliyo bora pale wanapostaafu kwa umri au kupoteza uwezo wa kujipatia kipato kwa njia ya ajira.
Pia tunafahamu umuhimu wa Mifuko ya hifadhi ya Jamii katika kuchangia maendeleo ya Taifa letu.
Pamoja naufahamu huo, ni matarajio yetu kuwa, katika miaka mitatu iliyobaki (2021 –2023) kuelekea mwisho wa Kipindi cha Mpito, Serikali itazingatia mapendekezo yake pamoja na Wadau namna bora ya kufikisha taarifa kwa Wanachama wa Mifuko bila kuleta taharuki na migogoro kama ilivyotokea zilipotangazwa Kanuni za 2018.
Ndugu Waandishi wa Habari TUGHE tunamalizia Tamko letu hili kwa kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassankwa namna alivyopokea hoja za Wafanyakazi na kuzitolea majibu yenye Matumaini makubwa wakati wa Sherehe za Mei mosi 2021 Kitaifa Jijini Mwanza.
Wafanyakazi tuliwasilisha hoja za kuomba nyongeza ya Mishahara, Mhe. Rais akapokea na kutoa ahadi ya Nyongeza Mwaka ujao 2022.
Tuliomba kupandishwa Madaraja yaliyokwama kwa muda mrefu, Rais akatoa maelekezo na sasa Watumishi wa Umma wanaendelea kupata haki yao ya Madaraja kwa mujibu wa Sheria.
Aidha, Vyama vya Wafanyakazi tulifikisha kilio cha uwepo Tozo ya 6% (Value Retantion Fee) wanayokatwa Wanufaika wa Mikopo yaElimu ya Juu kila Mwaka, hili nalo Mhe. Rais ameagiza liondolewe.
Hoja ya Wategemezi wenye umri wa Miaka 18 kuondolewa katika huduma za NHIF nayo ilipokelewa na Mhe. Rais ameagiza Umri wa Mtoto wa Mwanachama wa NHIF kuondolewa kwenye huduma za NHIF ni miaka 23 badala ya 18 ya awali ambayo iliwanyima Wanafunzi haki ya kupata huduma za Afya wakiwa wategemezi waWazazi wao.
TUGHE tunamshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuonesha nia njema kwa Wafanyakazi. Kwa niaba ya Wanachama wetu, tunaahidi kushirikiana na Mhe. Raispamoja na Serikali yake katika kutekeleza malengo tuliyojiwekea kama Taifa.
WITO: TUGHE tunahimiza Wanachama, Watumishi wa Umma na Wafanyakazi kote Nchini kuendelea kujituma na kufanyakazi kwa bidii nakukuza tija.
Tukifanya hivyo, tutakuza Uchumi wa Nchi na kuipa Serikali uwezo wa kuhudumia Jamii na kuwa na uwezo wa kuongeza ajira na kuboresha maslahi ya Wafanyakazi Nchini.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa na Baraza Kuu TUGHETaifa na kusomwa mbele ya Waandishi wa Habari na Nd. Archie Mntambo,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE)
“Huduma Bora, Maslahi zaidi”
Post a Comment