Kibaha, Pwani
Ujumbe wa Umoja wa Watengenezaji wa Magari Duniani (Association of African Automobile Segment-AAAM) ambao ni pamoja na kampuni za Nissan, Ford, Bmw, Isuzu, Toyita na Volkswagen, watembelea Kiwanda cha kisasa cha magari cha GFA Kilichopo kibaha mkoa wa Pwani hapa nchini.
Msafara wa Umoja huo wa Watengeneza magari duniani, umetembelea kiwanda cha GFA, ukuwa tayari umeshakutana na viongozi wa Serikali na kuzungumza mambo kadha katika kuhakikisha lengo la Tanzania ya Viwanda linatimia kwa vitendo
Katika kiwanda cha kutengeneza magari cha GFA Assemblers Mkurugenzi wa Kampuni ya Nissan ukanda wa Afrika, Mike Whitfield alisema watashirikiana na kiwanda hicho cha GFA Assemblers katika nyanja mbali mbali na kuweza kujitegemea na swala la uunganishwaji wa magari (Assemblies) na Tanzania inakuwa kama nchi zingine zinazotengeneza magari kama Afrika Kusini.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa Kampuni ya GFA Assemblers, Mehbooub Karmali alishukuru ujio huo wa msafara wa viongozi hao na kutanabaisha kwamba ujio wao ni neema kwao kama mambo yakienda vizuri basi serikali itakuwa inapata pesa za kigeni kufuatia magari kutengenezwa nchini hali itakayoongeza soko la ajira kwa vijana wengi wanao hitimu katika vyuo nchini.
Picha👇
Mshauri mkuu wa Waziri wa viwanda nchini Afrika ya kusini, Alec Erwin akizungumza jambo wakati wa ujumbe wa Umoja wa Watengenezaji wa magari Dunia(Association of African Automobile Segment (AAAM) walipotembelea kiwanda cha kuunganisha magari nchini kilichopo Kibaha mkoni Pwani. Kati kati ni Mwenyekiti wa bodi ya GFA Assemblers, Mehbooub Karmal na kulia ni Mwenyekiti wa umoja wa watoa huduma za mafuta na gesi nchini (ATOGS), Abdulsamad Abdulrahim. Jopo la viongozi wa Umoja wa Watengenezaji wa magari Dunia (Association of African Automobile Segment (AAAM) wakiangalia moja ya gari inavyotengenezwa katika kiwanda hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa GFA Assemblers, Mehbooub Karmali (kulia) akimtembeza moja ya wageni katika kiwanda hicho Kibaha mkoni Pwani
Post a Comment