"Hii ardhi yenu watu wanaitamani sana. Lakini niwaambie baada ya elimu urithi wa pili ni ardhi. Msikubali kuhadaiwa mtoe ardhi yenu kwa bei ya kutupa, ardhi yenu inathamani sana na mkiendelea kuitoa niwahakikishie mtajikuta mnatafuta kijiji cha kuishi maeneo mengine, na hii itaanza kuharibu hata asili yenu, mila na desturi zenu zitakufa, taratibu zenu na utamaduni wenu utaondoka, mtaitwa ni watu msio na kwenu, na mtaonekana ni watu wa ajabu. Msiruhusu watu kuchukua ardhi yenu kirahisi rahisi waje kwa mipango mahsusi." Katibu Mkuu Danie Chongolo akiwa Handeni, Juni 13, 2021. Bofya umsikilize Hapo👇
Post a Comment