Featured

    Featured Posts

WABUNGE KUSHIRIKI ASILIMIA 100 UHAMASISHAJI SENSA

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt  Albina Chuwa akiwaelezea wabunge kwamba katika Sensa ya mwakani watashirikishwa kwa asiimia 100 kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi lakini pia kujua mwenendo mzima wa Sensa kwani wao ni watu muhimu katika jamii. Ameyasema hayo wakati wa semina ya kuwapiga msasa kuhusu sensa katika Ukumbi wa Mkutano wa Takwimu jijini Dodoma Juni 19,2021.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akitoa shukrani kwa uongozi wa NBS kuwapatia wabunge mafunzo ya uelewa kuhusu sensa.


Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya wabunge waliohudhuria semina hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Alice Kaijage akichangia mada na kuuliza maswali wakati wa semina hiyo.
Mbunge wa Chaani Zanzibar, Juma Usonge Hamad akichangia mada kwa kutoa ushauri wa jinsi ya kuyashirikisha makundi mbalimbali katika jamii kufanikisha sensa.
Mbunge wa Viti Maalumu, Oliver Semuguruka akihoji kuhusu ni utaratibu gani utarahisisha kuwahesabu wageni hasa katika mikoa ya mipakani.
Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake Bungeni, Shally Raymond akifafanua jambo alipokuwa akiongoza semina hiyo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana