Featured

    Featured Posts

KATIBU MKUU CCM CHONGOLO AHITIMISHA ZIARA RUKWA , AANZA MKOA WA SONGWE

 

Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  Ndg Daniel Chongolo akiwa amembeba Mtoto Anastazia alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Nkasi   Julai 08,2021

Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (kulia) Ndg Daniel Chongolo akisikiliza maelezo  ya kifaa cha  .CT Scan toka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi dkt Martha Chacha, alipo tembelea hospitali ya Wilaya hiyo ,Kishoto ni mbunge wa Jimbo la Nkasi Ndg Vicente Mbogo,Julai 08,2021

 

Na Jacqueline Liana, Rukwa 
WAJUMBE wa sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, wameonya kwamba wao siyo viongozi wa kupiga porojo, na hawako tayari kuona ilani ikihujumiwa.

 
Katika taarifa yao ya kuhitimisha ziara ya siku mbili mkoani Rukwa, wajumbe hao wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, wamesema kwamba, katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2020-2021, hawatamvumilia
kiongozi au mtendaji serikalini atakayekuwa kikwazo katika kuitekeleza kwa ufanisi.

 
Wajumbe wengine ni Kanali mstaafu Ngemela Lubinga, ambaye ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Komredi Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Komredi Kenani Kihongosi.

 
Katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani humo, Julai 8, 2021, Komredi Chongolo alisema, ziara yao iliyoanza Julai 7 hadi 8, 2021, kutembelea mashina ya CCM wameshuhudia miradi
ambayo thamani ya fedha hailingani na viwango vya miradi husika.

 
Komredi Chongolo, alitoa mfano kwamba, hospitali za wilaya za Nkasi na Kalambo, kila moja imepatiwa sh. bilioni 2.3, lakini ujenzi wa miradi hiyo hauridhishi, kwa sababu thamini ya fedha hailingani na kazi iliyofanyika.

 
Kutokana na hali hiyo ya hovyo, Katibu Mkuu Chongolo, alimuagiza mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mheshimiwa Mkirikiti, kuhakikisha ndani ya siku zisizozidi 14 ujenzi wa hospitali hizo unalingana na thamani ya fedha, na kwamba maelekezo hayo siyo porojo.

 
“Tunamaanisha, siyo kurembaremba, ni lazima tufanye kazi yenye tija,” alisema Katibu Mkuu Chongolo katika kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi na watendaji wa CCM, viongozi na watendaji wa serikali, madiwani pamoja na wabunge.

“Wananchi wakiona mambo hayaendi, watatuona sisi tunapiga porojo, na sisi hatuko tayari kuitwa wapiga porojo,” alionya mtendaji mkuu huyo wa CCM.

Kero nyingine ambayo wananchi wanakumbana nayo ni ukosefu wa dawa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati, licha ya serikali kutoa fedha nyingi kuwezesha wananchi kupata huduma hiyo.

 
Katibu Mkuu Chongolo alisema kwamba, atawasiliana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, pamoja na uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD), kujua mamilioni ya fedha yanayotolewa kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa dawa yanakwama wapi.

“Tunataka watueleze nani anasababisha mkwamo katika upatikanaji wa dawa. Nasema hivi, sisi viongozi tunawajibu wa kufuatilia na kusimamia thamani ya fedha katika kila eneo,” alisema.

 
Alisema kwamba, kila kiongozi na mtendaji katika chama na serikali anawajibu wa kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha upatikanaji wa tija una kuwepo.

 
“Tutakuwa wakali, ni lazima tuogope fedha ya umma, ukizitumia vizuri zitakujengea heshima, ukizitumia vibaya zitakuvunjia heshima, hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mwadilifu,” alisisitiza.

 
Kuhusu migogoro ya ardhi, Komredi Chongolo alimwakigiza mkuu wa mkoa Mkirikiti, pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Rukwa kutafuta suluhisho la kero hiyo, ambayo imekuwa ikipoteza muda mwingi wa wananchi, ambao wangeutumia katika uzalishaji mali.

 
Kuhusu maji, Komredi Chongolo alisema bado ni changamoto, na kudokeza kwamba ni wakati muafaka kuanza kufikiria kuwa na mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Tanganyika kwa ajili ya mkoa wa Rukwa.

 
Kutokana na wananchi kulalamikia tatizo hilo, alilazimika kuzungumza na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambaye amemhakikishia kwamba atakwenda mkoani humo
kushughulikia tatizo hilo.

 
“Nadhani ni wakati muafaka, hebu tufikirie kuwa na mradi mmoja mkubwa wa maji katika ziwa Tanganyika kuweza kumaliza changamoto hii kwa muda mrefu,” alisema Komredi Chongolo.

 
Julai 9 hadi 10, Katibu Mkuu Chongolo, na wajumbe hao wa sekretarieti watakuwa na ziara ya kutembelea mashina ya CCM, katika wilaya za mkoa wa Songwe.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana