Featured

    Featured Posts

MBUNGE JANETH MAHAWANGA AAHIDI KUPAMBANA KUFA NA KUPONA KUHAKIKISHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI VYA KINAMAMA DAR ES SALAAM VINAPATA USAJILI VYOTE

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Juuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Ujoma wa Wanawake Tanzania (UWT) Janneth Mahawanga akizungumza wakati wa Kongamano la Kinamama Wajasiriamali  na Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha katika Jimbo la Ukonga, lililofanyika katika Ukubi wa Tembo, Check Point, Pugu Kigogo Fresh Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, jana.

Akizungumza, Mbunge huyo, ameahidi kuhakikisha anapambana kufa na kupona kuhakikisha Vikundi vya Kinamama hao vinasajiliwa vyote kwa mujibu wa sheria na pia kuhakikisha Wajasiriamali wa vikundi hivyo wanapata uwezo wa kutosha ili waweze kufanya shughuli zao kwa umahiri na kupata tija ya kutosha.

Alisema Kama Mbunge anayewakilisha mkoa wa Dar es Salaam, hilo ni jukumu lake muhimu kwa lengo la kuwaweka Kinamama pamoja na kushiriki kikamilifu kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika dhamira yake ya kuhakikisha  jamii inaimarika katika kiuchumi kupitia shughuli za Ujasiriamali za vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha.

"Kufuatia Mkutano wa Rais Samia na Wanawake wa Tanzania uliofanyika Dodoma Juni 8, 2021 na kuhudhuriwa na kundi kubwa la Wanawake wawakilishi ambao mimi nilikuwa miongoni mwao, Rais alizungumza mambo mengi ambayo yanalenga kumkoboa mwanamke kifikra na kiuchumi, kwa hiyo wajibu wangu kama mwakilishi wenu ni kuhakikisha agenda za mkutano ule nazileta kwenu na tuanze utekelezaji mara moja ndani ya mkoa wetu wa Dar es Salaam", akasema Mbunge Janneth.huku akianisha mambo aliyotaka Rais Samia yafanyiwe kazi.

Kuhusu Usajili wa Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo ya Fedha ambavyo awali vilitambuliwa kama VIKOBA, alisema elimu ya usajili wa vikundi hiyo inayofanyika kwa njia ya mtandao bado haijaeleweka kwa jamii na hivyo kusababisha vikundi vingi kufa kwa hofu.

"Seriakli yetu ni sikivu baada ya kulisemea hili Bungeni muda wa usajili umeongezwa hadi mwezi Novemba lakini pia imeendelea kuongeza jitihada kubwa  kupitia Halmashauri zetu kuhakikisha elimu hii ya usajili inafika kwa walengwa ili kumaliza taharuki iliyotanda mitaani., hivyo nawaomba sana tuzitumie ipasavyo fursa ambazo Rais amezianzisha ili kuimarisha uchumi wetu", akasema Mbunge Janeth Mahawanga.

Aidha alisema katika Kongamano hilo kwamba amebahatika kupata wadau ambao wapo tayari kushirikiana na wajasiriamali ambao wamekata tamaa kwa kukosa mitaji na kuwa kwenye foleni kwa muda mrefu kusubiri mikopo na kwamba kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu yeye na wadau hao wataanza Project ya 'Mwanamke wa Dar Tisha Mama, kwa nini Usiwe wewe' kwa kupata bidhaa moja kwa moja kutoka viwandani  bila kuwa na mtaji wowote na kwamba Project hiyo itafanyika chini ya  Taasisi ya  Tisha Mama Foundation na kwamba Projenct hiyo inatarajia kuanza mwanzoni mwa huo wa Oktoba katika majimbo yote  10 ya Dar es Salaam na Kata zote102 za mkoa huo na kuwaasa kinamama kuhakikisha awanaichangamkia fursa hiyo.

"Dar es Salaam ni Jiji la Kibiashara, Kinamama lazima mjue kuwa kuishi Dar es Salaam ni fursa tosha ya kuinika kiuchumi tuitumie fursa hii, Mimi ninaamini penye na pana njia na maenedeleo ya mkoa wetu yanaletwa na sisi wenyewe", akahitimisha hotuba yake Mbunge huyo Mwanamke Kijana Janet.

Katika Kongamano hilo ambalo ambalo Mbunge huyo aliliandaa kwa kushirikiana na NSSF na GS1 Tanzania, lilitanguliwa kwa wahamasishaji kutoa mada mbalimbali za kuchochea ujasiriamali katika nyanja za fedha na Bima, Wawezeshaji wakuu wakiwa ni Taasisi ya The Registered Trustees of Pegion Social and Charitable Trust (PSCT).

Taswira ya Kongamano hilo katika Picha
Baadhi ya Viongozi wa Vikundi vya Ujasiriamali na Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha akimsubiri Mbunge Janet Mahawanga kushuka kwenye gari lake baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo.

Mbunge Janeth Mahawanga akiongozana na viongozi hao kwenda ukumbiniMbune Janeth Mahawanga akiongozana na  Viongozi hao kuingia ukumbi wa Tembo lilimofanyika Kongamano hilo
Mbunge Janeth Mahawanga akiingia ukumbini na viongozi wenyeji.
Bunge Janeth akiwa na viongozi wa meza kuu ukumbini, Kushoto ni  Mkurugenzi wa  PSCT Kelvin Mmasi na kushoto kwa Mbunge huyo ni Mkurugenzi wa Kikundi cha Mindset Empower General Traders Rajab Sultan.
Mbunge Janet Mahawanga akionyesha furaha baada ya kuwasili ukumbini
Kiongozi wa wanavikundi Prisca Mutiganzi akifanya utambulisho wa vikundi mwanzoni mwa kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Kikundi cha Mindset Empower General Traders Rajab Sultan akizungumza.
Mbunge Janeth Mahawanga akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kikundi cha Mindset Empower General Traders Rajab Sultan
Wanakikundi cha Hakiki kutoka Kunduchi wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Mmoja wa wasaidizi wa Mbunge Janeth Mahawanga akiwa kwenye Kongamano hilo.
Msaidizi wa Mbunge Janeth Mahawanga akiweka mabo yake sawa wakati akiwa kwenye Kongamano hilo
Mwanasheria wa Taasisi ya PSCT Wakili Msomi wa kujitegemea Alice Mihayo akiwa kwenye Kongamano hilo 
Washiriki wakiwa kwenye Komnagamno hilo
Mkurugenzi wa  PSCT Kelvin Mmasi akitoa mada kuhusu ujasiriamali
Mhamasishaji akitoa mada
Erick Kafula kutoka GS1 Tanzania akitoa mada kuhusu alama za Barcon kwenye bidhaa
Erick Kafula kutoka GS1 Tanzania akitoa mada huku washiriki wakimsikiliza kwa makini.
Erick Kafula kutoka GS1 Tanzania akitoa mada

Mwanakikindi kutoka Ukonga akisoma risala

Mbunge Janeth Mahawanga akimshukuru msoma risala baada ya kukabidhiwa risala hiyo.

Mbunge Janeth Mahawanga akipongezwa na kupewa zawadi na wanakikundi

Mbunge Janeth Mahawanga akionyesha furaha wakati akipewa zawadi na kitenge na wanakikundi
Mbunge Janeth Mahawanga akihutubia kwenye Kongamano hilo
Mbune Janeth Mahawanga akionyesha cheti cha usajili cha kikundi pekee kilichopata usajili.
Mbunge Janeth Mahawanga akiendelea kusisitiza jambo wakati akihutubia kwenye kongamano hilo
Washiriki wakimshangili Mbunge Janeth Mahawanga kwa hotuba nzuri. Kisha akaselebuka nao wimbo wa 'Wanawake na maendeleo..." baada ya hotuba yake.



Wakampa zawadi tena Mbunge huyo


Mwanasheria wa Taasisi ya PSCT Wakili Msomi wa kujitegemea Alice Mihayo akitoa neno la shukrani kwa Mbunge Janeth Mahawanga.
Kiongozi wa wanakikundi akitoa neno la shukrani kwa Mbunge Janet

Kisha Mbunge Mahwanga akipigwa picha za kumbukumbu na viongozi na wanavikundi
















Mbunge Janeth Mahawanga akizungumza na mwanakikundi wakati akiondoka ukumbini.
Kisha akanunua bidhaa za mwanakikundi huyo.
Mbunge Janeth Mahawanga akiaga wanavikundi wakati akiondoka ukumbini
Mbunge Janeth Mahawanga akitoka ukumbini baada ya kongamano kumalizika kwa kishindo.
Mbunge Janeth Mahawanga akisindikizwa na baadhi ya viongozi wa vikundi wakati akiongoka ukumbini baada ya kongamano hilo. CCM Blog/Bashir Nkoromo/2021
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana